Waamini wajitolea kujenga Kanisa Tabora
KASI ya ujenzi wa Kanisa la Parokia ya Familia Takatifu Ipuli Jimbo Kuu
Katoliki Tabora unaendelea kwa kasi huku waamini wa parokia hiyo wakitarajia
kuukamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa.
Akizungumza na Gazeti hili
Paroko wa Parokia hiyo Padri Ponsiano Kibobera amesema wamefikia uamuzi wa
kujenga Kanisa hilo yakiwa ni matokeo ya ongezeko la kasi la idadi ya waamini
hali iliyosababisha Kanisa la zamani kutokabiliana na ongezeko hilo.
Padri Kibobera ameliambia
Gazeti hili kuwa Kanisa linaloendelea kujengwa ni matunda ya kazi ya waamini
wenyewe bila kupata msaada wowote toka nje hali inayoonesha ukomavu wa Imani
waliyoipokea miaka mingi iliyopita.
Aidha amesema wana parokia
wamejipangia kulijenga Kanisa kwa utaratibu wa jumuiya ndogondogo na vikundi
mbalimbali vya vyama vya kitume.
Kanisa hilo litawapatia
waamini fursa ya kujipatia eneo zuri, tulivu la wao kufika kwa ajili ya kusali,
kuomba, kumsifu na kumshukuru Mungu.
Padri Kibobera amesema mpaka
sasa ujenzi wa Kanisa hilo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 147, 000, 0000
za kitanzania. Kanisa hilo lipo katika
hatua ya msingi, na hadi linakamilika
litagharimu shilingi Bilioni 2 za kitanzania.
Parokia ya Familia Takatifu
Ipuli ilianzishwa mwaka 1972 na kukamilika mwaka 1983 chini ya uongozi wa
mapadri wa shirika la Wajezuiti waliokuwa na makao yao hapo Tabora.
Kanisa hilo likikamilika
litakuwa na uwezo wa kuchukua waamini 2500 waliokaa kwa wakati mmoja.
NIMEFURAHI KULIONA KANISA HILO KIUKWELI IPULI IMEKUWA KWA KASI SANA NA KANISA TULILOKUWA TUKITUMIA LILIKUWA DOGO, NA HAPO TULISHAHAMA KUTOKA MISUFINI AMBAPO NDIO KANISA LA PAROKIA LILIPOKUWA AWALI NA NDIO KANISA LANGU NILILOBATIZIWA , KANISA AMBALO LINAENDELEA KUTUMIKA NALO NILIWEZA KUPATIA SAKRAMENTI YA KIPAIMARA NAWAPONGEZA WANA FAMILIA WOTE YA IPULI KWA KAZI KUBWA MLIYOIFANYA MUNGU AWAONGEZEE MLIPO PUNGUZA. NAITWA JULIUS LUSWAGA WA KIGANGO CHA MAGEREZA PAROKIA YA IPULI KWA SASA NIPO PAROKIA YA WATAKATIFU WOTE NZUGUNI JIJINI DODOMA
ReplyDelete