Posts

Showing posts from March, 2019

Wanaume Katoliki DSM waanzisha Bima ya Afya, Maisha

Image
Askofu Mkuu Mwandamizi  wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Jude Thadeus Ruwaichi akimkabidhi Mwenyekiti wa UWAKA Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Ndugu Amedeus Mosha kadi za Bima ya Afya  mara baada ya kuzindua Mradi huo Dar es  Salaam katika sikukuu ya Mtakatifu Yosefu Msimamizi wa Wanaume Wakatoliki iliyofanyika katika  kituo cha hija Pugu (Picha na Philipo Josephat) Na. Philipo Josephat-Dar es Salaam U moja wa Wanaume wakatoliki wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam umeanzisha Bima ya Afya na Bima ya Maisha. Askofu Mkuu Mwandamizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mhashamu Yuda Thadei Ruwaichi amezindua kadi za Bima hizo hivi karibuni baada ya kuhitimisha Ibada ya Misa Takatifu siku ya wanaume katoliki (UWAKA) katika Sherehe ya Msimamizi wao Mtakatifu Yoseph iliyofanyika kwenye kituo cha hija Pugu   jiji Dar es Salaam.   Askofu Ruwaichi amewapongeza wanaume Katoliki Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam kwa ubunifu mkubwa wa kuanzisha Kampuni ya Bima ya

Mpwapwa wamuomba Rais Magufuli awatembelee

Image
Na Damasus Mtalaze, Kibakwe W akazi   wa wilaya   ya    Mpwapwa    mkoani    Dodoma   baada    ya   kuchoshwa   na   uharibifu wa   mazingira   katika    wilaya    hiyo   unaofanywa    zaidi   hasa   na   watu   wenye    fedha      wamemuomba    Rais   wa   Jamhuri ya   Muungano   wa   Tanzania   Mheshimiwa     John       Magufuli   afanye   ziara   wilayani   humo   ili   aelezwe    ni   kwa   jinsi   gani   wananchi   wa   wilaya   hiyo      wameshindwa     kushiriki     kuzuia     uharibifu   wa mazingira. Wakizungumza   na   gazeti     Kiongozi   kwa   nyakati   tofauti   wananchi   hao   waliokataa   kutaja   majina   yao   wamesema   kuwa   kama   hatua   za   dharura   hazitachukuliwa   mapema   na   wizara husika ama Kiongozi   wa juu katika serikali   yaani Rais   huenda     wilaya    hiyo    ya    Mpwapwa    ikawa jangwa kutokana   na   kuharibiwa   kwa   mazingira   hata   sehemu   ya   vyanzo   vya   maji. Uharibifu wa mazingira umeendelea kukithiri huku   serik