Posts

Showing posts from May, 2017

MAGAZETINI LEO JUMATANO MEI 31

Image

Kanisa Barani Afrika: Chombo cha haki, amani na upatanisho!

Image
Kardinali Fernando Filoni, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa watu wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Kupaa Bwana, Mbinguni, tarehe 25 Mei 2017, alikutana na kuzungumza na wakleri pamoja na watawa wa Jimbo Katoliki la Bata, huko Equatorial Guinea kwa kukazia utambulisho wao kama Kanisa familia ya Mungu inayowajibika, dhana iliyotiliwa mkazo sana katika maadhimisho ya Sinodi ya kwanza ya Maaskofu kwa ajili ya Kanisa la Afrika. Huu ni mwaliko wa kuendelea pia kushikamana na Kanisa la kiulimwengu katika mchakato mzima wa uinjilishaji, lakini kwa namna ya pekee na Askofu wao Juan Matogo Oyama. Kardinali Filoni anawapongeza wakleri na watawa kuwa mchakato mzima wa uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda wa huduma makini katika sekta ya elimu, afya, ustawi na maendeleo endelevu ya watu wa Mungu nchini Equatorial Guinea: dhamana, utume na asili ya Kanisa ambalo linatumwa na Kristo Yesu ili kuinjilisha. Uinjilishaji ni sehemu ya vinasaba vya maisha, utume na changamoto

MAGAZETINI LEO JUMANNE MEI 30

Image

WAWATA NA CARITAS WAWAPA MBINU WANAWAKE MBEYA

Image
  IMEELEZWA  kuwa wanawake ni nguzo ya familia,jamii na Taifa lolote duniani ,hivyo hawapaswi kujiona wanyonge  na badala yake  wajitume katika shughuli mbalimbali za kujipatia kipato bila kujibakisha ili waweze kuzilea vyema familia katika maadili mema  na hata kufikia hatua ya kulitegemeza Kanisa. Hayo yamesemwa na Mratibu wa Jinsia,,Vijana na  Watoto, Idara ya Caritas  na Maendeleo,Jimbo Katoliki la Mbeya,Praxeda Manyuka katika ziara yao ya kuwatembelea Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Moyo Mtakatifu  wa Yesu, Parokia ya Ilambo kujionea shughuli za maendeleo  wanazozifanya  ili kujiingizia kipato. Praxeda amesema kuwa  wanawake kama walezi wa familia  wanapaswa kujituma katika shughuli mbalimbali za kujitafutia kipato ili waweze kuilea vema familia,kaya  na kwamba wanao uwezo mkubwa wa kulitegemeza kanisa. "Akina mama ndiyo nguzo ya familia,mnapaswa kujituma katika shughuli mbalimbali za maendeleo...tunaamini mwanamke licha ya kuwa mzazi pia ni mlezi  na nguzo y