Posts

Showing posts from October, 2018

Ukuaji uchumi usioheshimu mazingira ni uasi-Ask. Banzi

Image
Na Pascal Mwanache, Korogwe I MEELEZWA kuwa uharibifu wa mazingira unaofanywa kwa jina la maendeleo na ukuaji wa uchumi ni uasi sawa na kuabudu miungu, huku wito ukitolewa kwa kila mwanadamu kusheshimu kazi ya uumbaji. Hayo yamesemwa na Askofu wa Jimbo Katoliki Tanga Mhashamu Antony Banzi katika Misa Takatifu ya kuwasimika viongozi wapya wa Shirika la Masista wa mama yetu wa Usambara (COLU) iliyofanyika katika Makao Makuu ya shirika hilo huko Kwamndolwa, Korogwe. Akitoa homilia yake katika misa hiyo Askofu Banzi amesema kuwa mwanadamu amepewa mamlaka juu ya mazingira huku akitakiwa kutumia zawadi ya akili na utashi katika kuutiisha ulimwengu na vilivyomo kwa manufaa ya leo na kesho. “Kuiheshimu dunia ni moja ya maadili na ni amri ya Mungu. Kuharibu mazingira ni kuabudu miungu. Tusiitumie dunia kwa fujo kwani atakayeathirika ni mwanadamu mwenyewe. Tukiitunza nayo itatutunza” amesema Askofu Banzi. Pia ametaka kuwepo kwa njia rafiki katika uvuvi na ufugaji wa nyuki, huku

Balozi wa Papa apongeza Kanisa katika mapambano dhidi ya mila potofu

Image
Na Veronica Modest, Serengeti B ALOZI wa Baba Mtakatifu nchini Askofu Mkuu Marek Solczynski   amelishukuru Kanisa Katoliki kwa kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya mila potofu, hasa ukeketaji wa watoto wa kike, ndoa za utotoni na ndoa za mitara. Akizungumza na Kiongozi mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kichungaji   ya siku 8 ndani ya Jimbo Katoliki Musoma balozi huyo amesema kuwa, kuna baadhi ya   udekano alizotembelea   na amekutana na changamoto kubwa ya kupewa taarifa ya kuwepo kwa vitendo vya ukeketaji wa watoto wa kike, ndoa za utotoni na ndoa za mitara ambazo zimekuwa changamoto kubwa kwa wakristo walio wengi hata kushindwa kupata sakramenti takatifu ya ndoa kutokana na kuwa na wake wengi. “Nimefika nimeona mimi mwenyewe kwa macho yangu ,nimesikia kutoka katika taarifa zilizowasilishwa kwangu na mapadri wa udekano wa Tarime, Rorya na Serengeti. Awali nilikuwa nasoma kwenye vyombo vya habari ila nimewaona na waamini wetu hivyo ninalishukuru kanisa kwa ku

MAMBO YA MSINGI KUHUSU KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 150 YA UKRISTO

Image
Wapendwa mapadri, watawa, walei napenda kuwafikishia rasmi taarifa juu ya kilele cha maadhimisho kitaifa ya miaka 150 ya uinjilishaji Tanzania bara. Kilele kitakuwa Bagamoyo: ·         Kuwasili Ijumaa  2.11.2018 ·         Semina/sala        3.11.2018 ·         Misa ya Kilele       4.11.2018 Mahali: Bagamoyo (Jimbo Katoliki la Morogoro), Mkoa wa Pwani. Mchango wa Kila Mshiriki: · Watu wazima ni shilingi laki moja na nusu (150,000/=).   · Watoto ni shilingi elfu tisini (90,000/=).   Kuhusu mchango wa ushiriki · Mchango utumwe kwenye namba akaunti ifuatayo: Jina la Akaunti: 150 JUBILEI KANISA KATOLIKI Namba ya Akaunti: 00111509958201 Jina la Benki: MKOMBOZI COMMERCIAL BANK PLC Benki Swift Code: MKCBTZTZ · Kivuli cha listi ya malipo itumwe kwa Ndugu Erick Mwelulila (0764025761/finance@tec.or.tz) Mkurugenzi wa Fedha na Utawala TEC. · Malipo yote yafanyike kwa njia ya benki Utoto Mtakatifu: Tukizingatia ukweli kuwa watoto wa utoto mtakatif