Posts

Showing posts from March, 2020

Maaskofu, mapadri, watakiwa kuhamasisha waamini kushiriki Kongamano la Ekaristi Takatifu

Image
MAjimbo ya Kanda (metropolitani) ya Magharibi yaaswa kuhamasisha zaidi waamini wao kwa namna ya pekee kwenye maandalizi ya Kongamano la nne la Ekaristi Takatifu kitaifa litakofanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora. Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paul Ruzoka hivi karibuni katika kikao cha saba cha maandalizi ya Kongamano hilo kilichohudhuriwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye   ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki   Mbeya. Akizungumza katika kikao hicho Askofu Ruzoka amewaomba wajumbe kutoka majimbo ya Tabora, Kahama, Kigoma na Mpanda kuwa mabalozi wa kuhamasisha waamini juu ya tukio hilo muhimu litakatolofanykika 1-5 July mwaka huu. Aidha amewakumbusha wajumbe kusali sala maalum katika majimbo   yote ya Tanzania   kuliombea Kongamano hilo. Vile vile ameagiza Kurugezi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Tanzania ihakikishe kwamba vyombo vya habari vya majimbo yote vinashirikishwa kikamili

Afya ya Baba Mtakatifu Fransisko inaimarika

Image
DR . Matteo Bruni Msemaji Mkuu wa Vatikani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, afya ya Baba Mtakatifu Fransisko   ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua makali inaimarika. Hivi karibuni Papa Fransisko alikumbwa na mafua makali ambayo yalimsababisha ashindwe kuhudhuria Mafungo ya Kwaresima 2020 kwa wasaidizi wa karibu wa Baba Mtakatifu, “Curia Romana” kuanzia Machi 1- 6 mwaka 2020 huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma. Kwa sasa Papa Fransisko anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatikani. Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia, nje kidogo ya mji wa Roma. Dr. Matteo Bruni amefafanua kwamba, Baba Mtakatifu anasumbuliwa na mafua ambayo hayana uhusiano wowote na magonjwa mengine. Tafakari wakati wa mafungo inaongozwa na Padri Pietro Enrico Bovati, SJ, Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa ya Biblia

‘Wajibu wa serikali ni kuangalia Raia wake’

Image
ASkofu wa Jimbo Katoliki   Rulenge-Ngara, Mhashamu Severine Niwe-Mugizi ameiomba serikali kusaidia baadhi ya vituo vinavyowasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwenye jamii.   Askofu Niwe-Mugizi ameyasema hayo Machi 2 mwaka huu wakati akifungua bweni la wasichana katika kituo cha watoto cha Nazareti kilichoko Nyamiaga, Wilaya ya Ngara mkoani Kagera. Hafla hiyo ilitanguliwa na tukio la kubariki vyumba vya bweni hilo. “Watoto wanaosaidika ni wa jamii ya Tanzania na hivi hata serikali inapaswa kufikiria pia nini inachoweza kufanya ili kusaidia huduma ya hiki kituo ili kiendelee,” Baba Askofu NiweMugizi huku akiongeza;   “Najua serikali ina mambo mengi sana lakini wakishaona kwamba kituo kinasaidia watoto wa Tanzania, wataweza kutuunga mkono. Inawasaidia hata wao kwa sababu ni wajibu wa kwanza wa serikali kuwahudumia hawa watoto. Serikali ndiyo inastahili kuwa mstari wa mbele katika kuangalia mahitaji ya raia wake na haswa watoto maana ukishawaacha waishi maisha