Posts

Showing posts from May, 2020

Prof Makubi: Corona bado ipo wananchi msibweteke

Image
MGanga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amewataka   wananchi waendelee kuchukua tahadhari   juu ya maambukizi ya ugonjwa wa covi 19 unaosababishwa na virusi vya corona. Prof. Makubi ameeleza hayo   hivi karibuni alipokuwa anazungumza na   Gazeti Kiongozi kuhusu kile kinachosadikiwa na jamii kuwa tayari kuna dawa ya corona. “Ninachiotaka kuwaambia wananchi ni kwamba, hakuna dawa ya corona. Mpaka sasa dawa haijapatikana nna ile tuliyoleta kutoka Madagascar bado inafanyiwa uchunguzi kujiridhisha. Wananchi hawa vijana na wale waishio vijijini wanapaswa waelewe kuwa,   virusi vya corona havibagui umri wala mahali. Vijijini corona ipo tena ni rahisi kusambaa hasa kwenye minada na magulio. Hivyo waendelee kuchukua tahadhari kama zinavyoelekezwa   na serikali pamoja na wataalamu wa afya   ikiwemo WHO. Amewataka wenyeviti wa Mitaa, Vijiji, kata nk. kuweka mikakati ambayo itawasababisha wananchi   waendelee na shughuli zao za kiuchumi.   “Kwa mfano minada inaweza kuongezwa kwen

Vyombo vya Kanisa vyatakiwa kuzipa kipaumbele habari za Covid-19

Image
KATIKA kukabilianana Covid-19, vyomba vya habari vinavyomilikiwa na Kanisa Katoliki, vimetakiwa kuzipa kipaumbele habari zinazohusiana na mapambano dhidi ya virusi vya corona husani zile zinazotia matumaini, kuondoa hofu na woga kwa wananchi. Rai hiyo imetolewa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Mhashamu Flavian Kasala, katika mahojiano Maalum na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Baraza hilo, yaliyofanyika katikati ya juma jijini Dodoma. Askofu Kasala amehimza vyombo hivyo kutumia hata lugha za asili pale inapobidi ili kuhakikisha ujumbe unaeleweka kwa makundi yote ndani ya jamii. “Ni kweli lazima tuwe na mashaka, lakini mashaka haya yanatakiwa kuwa yenye matumaini…kumbe vyombo vyetu virudishe hayo matumaini kwamba binadamu anaweza kupigana vita na kushinda na hili ndilo wazo letu kubwa,” amesema. Pia ametoa wito kwa vyombo hivyo vya habari, kuhakikisha vinautumia ulivyo ujumbe wa TEC kuhusu ugonjwa huo wa Corona hasa kwa kuendana na mazingira halisi ya

Tabora kuenzi ndoto za Padri Nyamiti kuanzisha chuo cha muziki

Image
KUFUATIA kifo cha Padri Prof. Charles Nyamiti kilichotokea Mei 19, 2020 katika Hospitali ya Mt. Anna Ipuli, Jimbo Kuu Katoliki Tabora limedhamiria kuendeleza ndoto za mtaalamu huyo wa muziki hasa za kuanzisha chuo cha muziki. Akizungumza na KIONGOZI mapema wiki hii Mratibu wa Idara ya Liturujia, Jimbo Kuu Katoliki Tabora ambaye pia ni mwanafunzi wa muziki wa Padri Nyamiti, Padri Deogratius Mwageni, amesema kuwa Padri Nyamiti alikuwa anatamani kuanzisha chuo cha muziki na yeye mwenyewe alikubali kujitoa ili aweze kufudisha nadharia ya muziki na vitendo. “Kwa kuanzia alikuwa na wanafunzi watatu ambao ni waseminari walioko likizo na mpaka siku ya mwisho kabla ya kifo chake alikuwa anafundisha muziki. Siku hiyo ya Jumatatu alifundisha kwa muda mrefu tena bila kuchoka mpaka alipoombwa apumzike. Ndipo akaenda kupumzika kidogo na akiwa mapumzikoni hali yake ilibadilika hivyo akapelekwa hospitali na baada ya vipimo akakutwa ana malaria kali” ameeleza Padri Mwageni. Ameongeza kuwa alil