Askofu Lebulu aadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Upadri
Na Sarah Pelaji, Same-Kisangara Juu A skofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha Mhashamu Josaphat Lebulu ameadhimisha Jubilei ya dhahabu ya Upadri yaani miaka 50 tangu alipopata Daraja Takatifu la Upadri. Jubilei hiyo imeadhimishwa Desemba 11 mwaka huu katika Parokia ya Kisangara Juu Jimbo Katoliki Same ambapo parokia hiyo pia imeadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na katika parokia hiyo ndipo Askofu Mkuu Mstaafu Lebulu alipewa Daraja Takatifu la Upadri na Askofu Joseph Kilasara Desemba 11 mwaka 1968. Katika maadhimisho hayo, Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Mhashamu Gervas Nyaisonga amesema kuwa, kwa niaba ya Maaskofu wakatoliki Tanzania, anampongeza Askofu Lebulu kwa kufanya kazi ya utume uliotukuka huku akimsihi aendelee kulisaidia Kanisa akitumia hekima na vipawa alivyojaliwa. “Ni wazi Askofu Lebulu amestaafu na anaadhimisha jubilei hii ya dhahabu lakini bado ana nguvu na anahitajika katika Kanisa. Sisi tunamuombea M...