Posts

Showing posts from April, 2020

Katibu Mkuu TEC: Wananchi msikebehi maelekezo ya serikali dhidi ya corona

Image
JAMII imetakiwa kutokuzikebehi na kuzibeza juhudi   zinazofanywa na serikali katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa hatari wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, badala yake itekeleze kwa vitendo maagizo na miongozo inayotolewa. Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Charles Kitima katika mahojiano maalum na vyombo vya Habari nchini, yaliyofanyika katikati ya juma ofisini kwake Kurasini jijini Dar es Salaam. Amesema, Kanisa Katoliki nchini linaridhishwa na hatua zinazofanywa na serikali kupitia Wizara ya Afya katika mapambazo dhidi ya ugonjwa huu ulionea sehemu mbalimbali duniani, hivyo akasisitiza kwamba hakuna sababu ya baadhi ya watu ama makundi ya kijamii kuzibeza na kuzikebehi juhudi hizo. Katika kusisitiza zaidi amesema “Tuiache Serikali ifanye kazi yake kwa kutumia wataalam wa afya iliyonao na kila mmoja kwa nafasi yake, atoe ushirikiano kama inavyotakiwa…hili siyo tatizo la kukebehi wala kufanyia mzaha kw

Kumbukumbu ya miaka 15 tangu Mt. Papa Yohane Paulo II afariki dunia

Image
KAnisa Katoliki duniani Aprili 2 mwaka huu linakumbuka miaka 35 tangu Papa Yohane Paulo II (sasa Mtakatifu) afariki dunia. Mtakatifu Yohane Paulo II alifariki dunia tAprili   2 mwaka 2005, yaani miaka 15 iliyopita na kuacha ushuhuda wenye mvuto katika maisha ya binadamu. Kardinali Angelo Comastri, Mhudumu Mkuu wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatikani akitoa ushuhuda wa maisha ya Mtakatifu Yohane Paulo II, kama sehemu ya kumbukumbu ya miaka 15 tangu Mtakatifu Yohane Paulo II alipofariki dunia ameeleza kuwa; Hata leo hii, katika hofu, wasi wasi na taharuki ya kuenea kwa ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na Virusi vya Corona, COVID-19, bado Kanisa linaamini kuwa Mtakatifu huyo   anaendelea kuiombea dunia na watu wa Mungu katika   dhoruba hii kali. Takwimu za maambukizi na vifo vinavyotokana na Virusi vya Corona inaonekana kuongezeka maradufu, kiasi cha kuwakatisha watu tamaa ya maisha. Watu wametikiswa kutoka katika undani wa maisha yao kiasi cha kuanza kukata

Utume wa Redio Maria Tanzania watua rasmi jimboni Musoma

Image
ASkofu wa Jimbo Katoliki   Musoma Michael Msonganzila, ameushukuru uongozi wa Redio Maria Tanzania kwa kufika Jimboni Musoma kurusha matangazo ,kwani ilikuwa ni kiu ya waamini wa Jimbo hilo kufikiwa na Utume huo kwa miaka mingi. Akizungumza wakati   kukabidhiwa   barua rasmi ya kutambulisha utume huo   na Mhamsishaji Mkuu wa Redio Maria Tanzania Emma Mahengo katika Jimbo hilo,Askofu huyo amesema kuwa ni zaidi ya miaka tisa waamini wakisubiri kwa hamu kubwa kufikiwa na Utume huo. “Imechukua miaka 8 hadi 9 tangu tuombe utume huu wa Redio Maria Tanzania katika jimbo letu. Leo hii   Machi 30 ,2020 tumepokea barua rasmi ya kutambulisha   utume huo kuanza hapa kwetu. Binafsi ns kwa niaba ya waamini nimefurahi sana kwa hatua hii ,na hata waamini wangu wamefurahi sana ,tuombe Mungu Mipango yote iende kama ilivyopangwa ndani ya mwaka huu,”amesema Askofu Msonganzila.   Mwakilishi Kiongozi wa Redio Maria Kanda ya Ziwa Stanslaus Mhema amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kurusha matanga