Utume wa Redio Maria Tanzania watua rasmi jimboni Musoma


ASkofu wa Jimbo Katoliki  Musoma Michael Msonganzila, ameushukuru uongozi wa Redio Maria Tanzania kwa kufika Jimboni Musoma kurusha matangazo ,kwani ilikuwa ni kiu ya waamini wa Jimbo hilo kufikiwa na Utume huo kwa miaka mingi.
Akizungumza wakati  kukabidhiwa  barua rasmi ya kutambulisha utume huo  na Mhamsishaji Mkuu wa Redio Maria Tanzania Emma Mahengo katika Jimbo hilo,Askofu huyo amesema kuwa ni zaidi ya miaka tisa waamini wakisubiri kwa hamu kubwa kufikiwa na Utume huo.
“Imechukua miaka 8 hadi 9 tangu tuombe utume huu wa Redio Maria Tanzania katika jimbo letu.
Leo hii  Machi 30 ,2020 tumepokea barua rasmi ya kutambulisha  utume huo kuanza hapa kwetu. Binafsi ns kwa niaba ya waamini nimefurahi sana kwa hatua hii ,na hata waamini wangu wamefurahi sana ,tuombe Mungu Mipango yote iende kama ilivyopangwa ndani ya mwaka huu,”amesema Askofu Msonganzila.
 Mwakilishi Kiongozi wa Redio Maria Kanda ya Ziwa Stanslaus Mhema amesema kuwa kwa sasa wamejipanga kurusha matangazo nchi nzima na Jimbo la Musoma ni mojawapo ,hivyo waamini wawe tayari kuipokea redio hiyo na kushirikiana katika kuiwezesha ili iendelee kufanya Utume wake.
Maparoko walioshiriki Misa Takatifu  iliyorushwa live na Redio Maria jimboni humo,Paroko wa Parokia ya Kigera Padri Robert Luvakubandi,Paroko wa Musoma Mjini Padri Benedict Luzangi,Paroko wa Parokia ya Mwisenge Padri Valence Matungwa na Paroko wa Parokia ya Rwamlimi ,pamoja na masista wa Moyo safi wa Afrika wa Jipe Moyo  wameishukuru timu ya redio kwa ,kufika katika parokia hizo na kurusha matangazo yao moja kwa moja.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU