Posts

Showing posts from January, 2017

Matokeo ya Kidato cha Nne 2016 yametoka

Image
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016. Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26. Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015. Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60. Kwa upande wa masomo, amesema ufaulu katika masomo ya History, Geography, Kiswahili, English Language, Basic Mathematics, Physics, Biology, Commerce na Book keeping umepanda kwa kati ya asilimia 0.12 na 8.08 ikilinga

Habari zilizopo katika magazeti ya leo jumanne ya January 31

Image

Habari zilizopo kwenye magazeti leo Jumatatu Januari 30

Image

‘Sheria ya habari isikiuke tunu za Kanisa’ Ask. Msonganzila

Image
WITO umetolewa kwa Waandishi wa habari wa Kanisa Katoliki kuhakikisha wanaendelea kutangaza Habari Njema kwa kutumia vyombo vya habari, kwa kufuata sheria na taratibu za nchi   huku   wakizilinda tunu za Kanisa zisitikiswe na   sheria mpya ya huduma ya habari ya mwaka 2016. Hayo yamesemwa   na Askofu Michael Msonganzila wa Jimbo Katoliki Musoma katika kikao   cha dharura cha Wakurugenzi   wa Mawasiliano majimboni na Wakurugenzi wa Vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki nchini kilichofanyika Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), kurasini, jijini Dar es salaam . Awali amewapongeza   wanahabari wa Kanisa Katoliki   kwa majukumu makubwa na magumu ya uinjilishaji waliyo nayo.   “Mnaifanya kazi hii katika nyanja mbalimbali za jamii, ninyi ni wainjilishaji nambari moja   katika Kanisa na kama ukitaka kuielezea   biblia ama   habari njema   na kuwafikia watu kwa urahisi   ni kupitia viganja vyenu, kalamu zenu na karatasi zenu… Tunaona watu wana kiu kubwa ya kupata taarifa m