Asilimia 70 ya walimu wanaidai serikali

IMEELEZWA kuwa asilimia 70 ya walimu wanaidai serikali ambapo kuanzia mwaka wa fedha 2013/2014 mpaka Desemba 2016, walimu walikuwa wanadai shilingi trilioni 1.185 sawa na trilioni 1.19.
Hayo yameelezwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama Cha Walimu Tanzania CWT, Ezekiah Oluoch katika mkutano wake na waandishi wa habari hivi karibuni, na kubainisha kuwa madai hayo ya walimu yanaathiri shule kwa kuwa walimu wanapaswa kufanya kazi na akili zilizotulia, hivyo wanapokuwa na madeni mengi ari ya utendaji wao inashuka.
“Mchanganuo huu wa madeni umechangiwa kwa kiasi kikubwa na walimu waliostaafu ambao wako 6,044 ambao hawajalipwa shilingi bilioni 556 ambazo zinapaswa kulipwa na PSPF. Lakini PSPF imeshindwa kuwalipa kwa sababu serikali haijapeleka fedha za walimu hawa katika mfuko wa PSPF” ameeleza Ezekiah.
Aidha amesema kuwa walimu waliopandishwa madaraja mwaka 2016 ni 85,945 na wanadai shilingi bilioni 301, na kwamba deni linakua kila mwezi kwa kiwango cha bilioni 25 ambapo endapo halitalipwa hadi kufikia Juni 2017, deni litakuwa limeongezeka kwa shilingi bilioni 150.
Pia Ezekiah ameiomba serikali kuongeza walimu kwani kuna upungufu mkubwa wa walimu katika shule mbalimbali nchini ili hali kuna walimu waliohitimu mafunzo yao na hawajaajiriwa bado.

“Tuna upungufu mkubwa sana wa walimu shuleni. Hii inatokana na walimu elfu 40 wako mtaani wanasubiri ajira, serikali haijawaajiri kwa kigezo cha kuhakiki vyeti” ameeleza.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU