Kilwa Chimbuko la Utawa Tanzania

KATIKA makala mojawapo niliwahi kuandika kuwa wakristo wa kwanza Afrika Mashariki walibatizwa Kilwa. Historia ilionesha kuwa Wareno walipofika Kilwa kisiwani kuanzia 1505 chini ya Francisco D’Almeida na askari kama 500 waliitiisha Kilwa.
Wafransiskani waliokuwepo kwenye meli hiyo walishuka wakaingia Kilwa Kisiwani wakasimika msalaba na waliimba wimbo wa kumsifu Mungu yaani Te Deum. Kishapo askari wa Kireno walishambulia Kilwa Kisiwani, waliiba na kuharibu mji.
Katika mazingira hayo wananchi 40 waliomba kubatizwa na wakabatizwa.  Kwa yeyote mwenye mawazo ya kihistoria atajiuliza hao walikuwa ni akina nani na walitoka wapi? Maswali mengi yalibaki kichwani mwangu.
Utafiti wangu wa kihistoria umegundua kuwa Sultani wa kwanza wa Kilwa Kisiwani, Ali Hasani Shiraz toka Uajemi kwenye miaka ya 960 hadi 1000 Mwaka wa Bwana aliweka makao yake Kilwa Kisiwani. Mmoja kati ya wake zake alikuwa ni mama wa Ki Ethiopia ambaye alikuwa mtumwa. 
Historia imegundua kuwa baadhi ya majina ya nasaba za masultani waliotawala Kilwa baada ya Shiraz kufa kuanzia 1022 hadi 1499 yalikuwa na majina ya Kiyahudi kama vile Ibrahimu, Suleiman na Dawudi.  Hata sultani wa mwisho kuondolewa na Wareno 1505 aliitwa Ibrahim Suleiman. Majina haya yanaashiria aina ya ukristo wa Kiyahudi.
Tafiti hizi zinathibitisha kuwa Yule Mama wa Ethiopia mtumwa huenda alikuwa ni mkristo wa kanisa la Ethiopia ambalo katika kipindi hiki lilifikia kilele cha kiutawala na walikuwa na koo zenye kudai nasaba ya Mfalme solomoni wa Yerusalem kuanzia wakati wa koo za Kizagwe kwenye mika 1000 mwaka wa Bwana hadi 1974.
Duru hizi zinathibitisha kabisa huko Kilwa Kisiwani kipindi hicho kulikuwa na ukristo wenye asili ya kanisa la Ethiopia. Tusishangae sasa kwa nini wakati wa Wareno watu 40 waliomba kubatizwa.
Mtafiti mwingine mwenye asili ya Kifaransa aliyeanza utafiti wake 2009 amebaini kuwa baadhi  ya maandishi yaliyopatikana Kilwa Kisiwani kwenye baadhi ya milango yanaashiria hapo Kilwa iliishi jumuiya ya wakristo.  Mtafiti huyo anadai kuwa hiyo Jumuiya ilikuwa ni jumuiya ya kimonaki ambao huenda walitoka Siria.
Mtafiti huyu, duru za kinasaba za Kilwa na wale waliobatizwa 40 wakati wa Ureno vinathibitisha kuwa Kilwa Kisiwani kabla ya Wareno kulikuwa na Jumuiya wakristo.
Hivyo ninaweza kusema pasina shaka  Kilwa ni chimbuko la Ukristo Tanzania. Kilwa ni chimbuko la Utawa na umonaki Tanzania.  Ni jambo la ajabu pia kabla ya kuzaliwa kwa Ndanda na Peramiho 1931 eneo  lote liliitwa Jimbo la  usimamizi la  kitume la Lindi. Tanzania sasa kuna monasteri za akina Baba nne katika lilioitwa Jimbo la usimamizi la kitume la Lindi na zaidi ya  kumi ya mashirika ya masista.
Kilwa ni chimbuko la umonaki Tanzania. Kanisa la Tanzania na hasa Jimbo la Lindi kutafuta namna ya kuenzi Kilwa kama chimbuko la Ukristo Tanzania. Ni muhimu sana tujifunze kwa kina Historia ya kanisa la Afrika. Kilwa ni sehemu muhimu sana ya chimbuko la ukristu Tanzania.
0784306170


Comments

  1. SIJAWAHI KUMUONA MWANDISHI MSHAWISHI MUONGO KAMA HUYU
    ALIEANDIKA MAKALA HII

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU