Jubilei ya Miaka 100 ya upadri kufungwa Dodoma

JIMBO Kuu Katoliki Dodoma limeteuliwa kuwa mwenyeji wa kilele cha Jubilei ya miaka 100 ya Upadri Tanzania  tangu padri wa kwanza mwafrika kupewa daraja takatifu ya upadri mnamo mwaka 1917.

Hayo yameelezwa na Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida hivi karibuni alipokuwa akiadhimisha ibada ya misa takatifu ya kutoa Daraja Takatifu la Ushemasi wa mafrateri wawili wa Shirika la Wamisionari wa Damu azizi ya Yesu Kanda ya Tanzania , iliyofanyika katika parokia ya amu Azizi ya Yesu Itigi Singida.

Mafrateri waliopewa daraja Tajatifu la Ushemasi ni pamoja na Frateri Dominic Mavulla na Frateri Alesandro Manzi,

Askofu Mapunda amesema kuwa ni heshima kubwa iliyotolewa katika Metropoliani ya Dodoma ambayo inaundwa na majimbo matatu ambayo ni Jimbo kuu katoliki Dodoma, Jimbo katoliki Singida na Jimbo Katoliki Kondoa , hivyo wana kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa zawadi hiyo ya kuwa mwenyeji kilele cha Jubilei ya mIaka 100 ya upadrI.

Amesema kuwa mbali na majimbo mengi kutindikiwa na mapadri lakini wana sababu ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hali iliyopo kwa sasa kwani hadi sasa ni majimbo machache yenye uhaba mkubwa wa watendakazi katika shamba la Bwana.

Hata hivyo amesema kuwa mbali na Jubiulei hiyo ya miaka 100 ya upadri pia mwaka 2018 Kanisa la Tanzania bara litaadhimisha Jubilei ya miaka 150 tangu ukristo ulipoingia Tanzania na jubilei hiyo itafanyika Bagamoyo.

Askofu Mapunda amesema kuwa kilele cha maadhimisho hayo itakuwa ni Agosti 15 mwaka huu 2017 katika Jimbo Kuu Katoliki Dodoma katika sikukuu ya Bikira Maria Kupalizwa Mbinguni ambapo mapadri wa kwanza  waafrika  walipadirishwa  Agosti 15 mwaka 1917.

Akizungumza katika ibada hiyo Askofu Mapunda alisema kuwa Jubilei ni zawadi kutoka kwa mwenyezi mungu hivyo waamini wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa zawadi ya wamisionari waliokuja Tanzania kwa ajili ya kuhamasisha vijana kujiunga na utume na hatimaye kuwapata mapadri.

Amesema kuwa, Kanisa bado linauhitaji mkubwa wa mapadri hivyo amewataka waamini kuendelea kuliombea Kanisa katika hitaji hilo ili uinjilishaji uendelee katika vizazi vya sasa na vijavyo .

Amesema kuwa mfano wa mamajusi ni mfano bora na wa kuigwa kwani wanatufundisha kumtafuta Mungu kwani wao walikuwa wanafanya hija ya kiroho katika nyakati tofauti tofauti kumtafuta Yesu Kristo kila mmoja kwa wakati wake na kumwabudu.

"Mamajusi walizunguka huko na huko walivuka mabonde, milima na mito katika kuifuta nyota ambayo ilikuwa inawapeleka kumwona Mtoto Yesu alipokuwa amelazwa baada ya kuzaliwa kwake" aliongeza Askofu Mapunda

Hata hivyo Askofu Mapunda amewataka waamini kujenga tabia ya kufanya hija za kiroho na watambue kuwa katika shughuli zote za kila siku wanaongozwa na nyota mbalimbali kwa mfano uuguzi, upadri na hata utangazaji wa neno la Mungu.


Amesema kuwa watu wengi wana njaa ya kiroho na watu wengi wanauliza ni wapi watapata mponyaji hivyo amewataka pia mapadri kuwa ni mkombozi wa wanaohitaji uponyaji huo.

Aliwataka kuzisome alama za nyakati  na kuzifahamu na kuwataka kuenenda kujifunza mahangaiko ya watu kama mwanzilishi wa shirika hilo Mtakatifu Gaspar Del Buffalo alivyokuwa na hamu hiyo.

Awali akimpokea shirikani Frateri  Domonic Mavula Mkuu wa Shirika Proviensi ya Tanzania Padri Chesco Peter Msaga alimtaka kuwa mwanga na nuru ya kuwaongoza wengine kuvuka kutoka kwenye giza.

Alisema kuwa Dira ya Kanisa kwa sasa ni kuhubiri neno la Mungu na kazi hiyo inapaswa kuenziwa kwani imeanza kufanyika miaka 100 iliyopita na ilikuwa ikifanywa na wamisionari waliokuja barani Afrika na Tanzania kwa ujumla kuendeleza kazi ya uenezaji wa neno la Mungu.

Padri Msaga alisema; “Wamisionari walikuja Tanzania kutuondoa katika utumwa wa vifungo vya giza la dhambi na kutuwezesha kumwabudu Mungu wa kweli.

Wamisionari walikuja kwa lengo la kutoa huduma ndani ya Kanisa na kuwasaidia wenye shida za kiroho,” Aliongeza Padri Msaga.

Akitolea mfano wakati wa mkutano uliofanyika huko amerika amesema kuwa mkutano huo baada ya kuulizwa nini mpango kazi wa Kanisa la Tanzania kwa kipindi cha miaka kumi alisema kuwa wao walisemakuwa mpango kazi wa Kanisa la Tanzania kwa miaka kumi ni kutangaza habari njema ya wokovu na kutangaza mwaka  wa bwana uliokubalika, kuwatangazia wafungwa habari njema ya kufunguliwa kwao  na kuwahubiria maskini habari njema ya wokovu,


Hilo ndilo jukumu la padri na kila muumini katika nyakati hizi.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU