Majadiliano ya kiekumene hayakwepeki: Askofu Ruzoka asisitiza

JIMBO Kuu Katoliki Tabora linaendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene ili kujenga na kudumisha majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Wakristo.

Askofu Mkuu Paul Ruzoka wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, katika mahojiano na gazeti hili hivi karibuni amesema kuwa,  majadiliano ya kiekumene ndani ya Kanisa ni kati ya mada zilizojadiliwa na kutolewa maamuzi na Sinodi ya kwanza ya Jimbo Kuu Tabora iliyoadhimishwa hivi karibuni kwa kuongozwa na kauli mbiu “Yesu hu seba” yaani “Yesu ni taa ya uhai wa  imani yetu.”

Kanisa linatambua kwamba, Kristo Yesu ndiye muasisi wake na kwamba, aliunda: Kanisa moja, Takatifu, Katoliki na la Mitume. Kumbe, majadiliano ya kiekumene miongoni mwa Makanisa ni jitihada za kutaka kujenga na kudumisha umoja wa Kanisa kama Kristo mwenyewe alivyoliombea, liwe na umoja. (Rej. Yn. 17: 21) Ikumbukwe kwamba, asili ya Kanisa ni moja,”ameeleza Askofu Mkuu Ruzoka,

Aidha amesisitiza kuwa, Maaskofu Mahalia kwa kushirikiana na Khalifa wa Mtakatifu Petro wanapaswa kukoleza ari na moyo wa majadiliano ya kiekumene yanayojikita katika: ushuhuda wa imani yao kwa Kristo na Kanisa lake hata kiasi cha kumwaga damu yao; ushuhuda wa sala na maisha ya kiroho kwa kusali na kutafakari pamoja Neno la Mungu linalopaswa kuwa ni dira na mwongozo wa maisha ya Wakristo pamoja na kushikimana kwa dhati katika kuwahudumia maskini na wale wote wanaosukumizwa pembezoni mwa jamii.
Askofu Mkuu Ruzoka anaendelea kufafanua kwamba, juhudi za majadiliano ya kiekumene zilianza tangu wakati wa maadhimisho ya Mtaguso wa Pili wa Lyon mnamo mwaka 1276; Mtaguso wa Florence wa Mwaka 1437, lakini maadhimisho yote haya hayakuweza kuzaa matunda ya umoja wa Kanisa.
Mababa wa Mtaguso Mkuu wa Pili wa Vatikani, wakaamua kuivalia njuga changamoto ya majadiliano ya kiekumene; dhamana iliyoendelezwa kwa namna ya pekee na Mtakatifu Yohane XXIII, Mwenyeheri Paulo VI, Yohane Paulo II, Benedikto XVI na kwa sasa kasi ya majadiliano ya kiekumene imeongezeka zaidi chini ya uongozi wa Baba Mtakatifu Fransisko.
“Kwa namna ya pekee kabisa, Jimbo Kuu Katoliki Tabora lilihamasika kwa maneno ya Mtakatifu Yohane Paulo II wakati wa maadhimisho ya Jubilei Kuu ya Miaka 2000 ya Ukristo aliyelitaka Kanisa kuwa ni chombo cha msamaha, haki, amani na upatanisho, ili kuponya dhambi na madonda ya utengano miongoni mwa Wakristo, ili kweli maadhimisho ya Millenia ya tatu ya Ukristo yaweze kuwa ni chachu ya msamaha, upatanisho na umoja wa Kanisa.

Hii ni changamoto pia iliyokuwa imefanyiwa kazi na Mababa wa Sinodi ya kwanza ya Afrika na hatimaye, Papa Yohane Paulo II akachapisha Wosia wa Kitume, Kanisa Barani Afrika, “Ecclesia in Africa” akiitaka Familia ya Mungu Barani Afrika kujikita katika Uenezaji wa Injili unaofumbatwa katika utamadunisho, majadiliano na mchakato wa maendeleo endelevu ya binadamu: kiroho na kimwili, daima Kanisa likiwa ni sauti ya wanyonge,” amesema.

Jimbo Kuu Katoliki Tabora linaendelea kutekeleza maazimio ya Sinodi ya kwanza ya Jimbo masuala mbali mbali yaliyobainishwa katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene.
Hii ikiwa ni pamoja na kushiriki katika Juma la Sala kwa ajili ya Kuombea Umoja wa Wakristo, kuanzia tarehe 18 - 25 Januari, wakati wa maadhimisho ya Siku kuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo, Mwalimu na mtume wa mataifa. Lengo ni kuwajengea waamini uwezo ili kweli waweze kuwa ni mashuhuda na vyombo vya huruma ya Mungu sanjari na kuongeza ushirikiano na mshikamano katika medani mbali mbali za maisha.

Pia amebainisha kuwa, Jimbo kuu la Tabora limejiwekea utamaduni wa kusali pamoja na Wakristo wa Madhehebu mbalimbali wakati wa Jumatatu ya Pasaka na Siku kuu ya Noeli, ili kuweza kuimarisha imani, mwingiliano katika maisha ya ndoa na familia, ili familia ziweze kushiriki kikamailifu katika maadhimisho ya Mafumbo ya Kanisa kwa kufuata taratibu, kanuni na sheria zilizowekwa na Mama Kanisa.

Hii pia ni dhamana ya kuimarisha ushiriki wa wazazi katika malezi na makuzi ya watoto wao kadiri kanuni msingi, maadili na mwanga wa Injili.

Comments

  1. Kwa karibu mwaka mmoja, mume wangu aliniacha mimi na watoto wetu wawili. Aliacha kujali, akaacha kupiga simu, na akaondoka kabisa. Nilikuwa nimevunjika moyo, nimechanganyikiwa, na karibu kupoteza tumaini. Kisha siku moja, rafiki yangu aliniambia kuhusu Dkt. Dawn, mtu wa kiroho aliyepewa kipawa na ulimwengu ili kuwasaidia watu kurejesha upendo na amani.

    Mwanzoni, nilikuwa na shaka, lakini kitu kuhusu maneno yake kilinipa amani. Aliniambia haswa kilichokuwa kibaya na kwamba mtu alikuwa ametupa uchawi mkali kututenganisha. Aliandaa kazi maalum ya kiroho na uchawi wa kuungana tena kwa ajili yangu - na ndani ya siku chache, mume wangu alinipigia simu ghafla, akilia na kuomba msamaha.

    Tangu wakati huo, maisha yangu hayajawahi kuwa sawa. Ndoa yetu sasa ni tamu na yenye furaha zaidi duniani. Tunapendana zaidi kuliko hapo awali, na nyumba yetu imejaa vicheko na baraka.

    Lakini sio hivyo tu - Dkt. Dawn pia alisaidia kuondoa bahati mbaya na nishati hasi iliyozunguka familia yetu. Tangu wakati huo, kila kitu kimekuwa laini: amani nyumbani kwetu, maendeleo ya kifedha, afya njema, na furaha safi.

    Ninashukuru ulimwengu kila siku kwa kuniongoza kwa Dkt. Dawn. Kwa kweli ni mtu mwenye nguvu na mwanga wa kimungu. Ikiwa unapitia hali yoyote - huzuni, bahati mbaya, au kuchanganyikiwa - usikate tamaa. Mfikie na uache ulimwengu ufanye kazi kupitia yeye ili kubadilisha hadithi yako, kama vile alivyobadilisha yangu.

    Wasiliana naye kwenye WhatsApp: +2349046229159 dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete
  2. Uchawi wa mapenzi wa Dkt. Dawn hufanya maajabu kweli.

    Niliwasiliana na Dkt. Dawn wakati uhusiano wangu ulipovunjika kabisa. Mpenzi wangu wa zamani alikuwa ameniacha na kunizuia kwenye mitandao yote ya kijamii. Nilivunjika moyo na kupoteza tumaini. Baada ya kushauriana na Dkt. Dawn, kila kitu kilibadilika. Mpenzi wangu wa zamani alirudi peke yake, akaomba msamaha kwa dhati, na akaomba msamaha. Leo, tunaishi pamoja kwa furaha, na hata tuna mtoto.

    Maneno hayatoshi kuelezea jinsi ninavyoshukuru. Kutokana na uzoefu wangu, naweza kusema kwa ujasiri kwamba Dkt. Dawn ni halisi, anayetegemewa, na mwenye nguvu. Ikiwa unakabiliwa na hali yoyote ngumu maishani mwako hivi sasa, Dkt. Dawn anaweza kukusaidia.
    ANAWEZA KUKUSAIDIA KWA MATATIZO YAFUATAYO:
    Kurudisha ndoa na mahusiano yaliyovunjika
    Kuvutia mafanikio na ukuaji katika biashara
    Matatizo ya uanaume, utasa, na ukosefu wa watoto
    Kurejesha mali zilizoibiwa au zilizopotea
    Kurudisha kazi zilizopotea au fursa za kazi
    Kinga dhidi ya uchawi na macho mabaya
    Hirizi za mvuto
    Kutatua migogoro ya ardhi na mali
    Kuwafanya wapenzi kutimiza ahadi zao
    Kushinda kesi mahakamani, na mengine mengi
    Huu si ulaghai — ni ushuhuda kutoka kwa uzoefu.
    Kwa maelezo zaidi, wasiliana naye moja kwa moja kwenye WhatsApp. +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI