Mapadri msiogope kusema na kusimamia ukweli -Askofu Niwemugizi

“DAIMA msiogope kuusema ukweli ambao utawaweka watu wa Mungu huru na kutoka katika mwenendo mbaya usiompendeza Mungu.”

Askofu Severine NiweMugizi wa Jimbo Katoliki Rulenge Ngara  ametoa mwito huo kwa mapadri wakati wa Misa maalumu ya kutoa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Shemasi Alex Blandi.


Akiwatia moyo Mapadri, Askofu Niwe-Mugizi amesema kuwa, msemakweli daima maisha yake yako hatarini lakini wajue utume wao wameukabidhi mikononi mwa Mungu ambaye atawaongoza na kuwavusha kwa kila vikwazo hasa vitokanavyo na kusema ukweli.

"Mpendwa Shemasi Alex na Mapadri kuweni wajasiri kwa kusema ukweli. Najua kuna watu wasiopenda kuusikia ukweli na mkweli daima huchukiwa na maisha yake yamo hatarini, yawekeni maisha yenu mikononi mwa Mungu matahifadhiwa naye," amesema.

Aliwahimiza mapadri daima kuwa wavumulivu, wenye subira, wenye kusamehe wasiokata tamaa . Pia  kuwa wabunifu kwa kuwa na muda wa kusema na muda wa kunyamaza.

Aidha Askofu Niwemugizi alielezea hali ambayo iliandikwa kwenye vyombo kadhaa vya habari kuwa yeye anaonekana wazi kumpinga Rais Magufuli juu ya suala la kutangaza uwepo wa njaa au ukame .

Alisema yeye binafsi hana ugomvi na Magufuli na kwamba anampenda sana kutokana kuwa miongoni mwa watu wanaosema ukweli na pia kusema wazi kuwa anapendezwa naye na utendaji kazi wake

Amesisitiza juu ya miito huku akisema kuwa, wazazi wengi hawatambui miito ya watoto wao na hivyo wamekuwa wakishindwa kuwaendeleza hasa wanapoelekea kuwa na wito wa kumtumikia Mungu kama Mapadri.

Alihimiza familia kuwa chanzo cha miito mitakatifu ya Upadri na Utawa na kuacha kutamani wito wa ndoa.

"Nawasihi wazazi heshimuni miito ambayo Mungu amewaitia watoto wenu na hasa miito hii ya Upadri na Utawa ambayo wengi wenu hamuipi kipaumbele kwa kudhani kuwa mtoto akiwa Padri au Mtawa mtakosa wajukuu. Kumbukeni miito hii ni sadaka yenu kwa Mungu," amesema.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU