Posts

Showing posts from October, 2016

MAGAZETINI LEO JUMATATU OKT 31

Image

UFAFANUZI BODI YA MIKOPO

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017. Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu. Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza. Katika mkutano na waandishi wa habari jana (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupok

MALEZI IMARA:”MAWILI HAYA” ndio,ila wewe zaidi.

Image
Tumeshuhudia kauli mbalimbali za majuto toka kwa baadhi ya watu wakidai kuwa isingekuwa baba, mama, kaka au rafiki yangu yule maisha yangu yasingekuwa hivi. Lakini pia tumesikia kauli za kutia moyo za watu waliofanikiwa na kudai kuwa ni kwa sababu ya fulani nina maisha mazuri hivi, nisingemsikiliza ningeharibikiwa maisha. Kauli hizo   hapo juu ni uthibitisho kuwa   malezi imara ni matokeo ya muunganiko wa ushauri wanaotupatia watu mbalimbali, athari za jamii inayotuzunguka na mwishowe lile mtu mwenyewe baada ya kupokea hayo mawili analoona ni muhimu kulizingatia. Mambo haya matatu ni lazima yawekwe pamoja ili kumsaidia mtu kuwa na maamuzi bora na mwishowe kuwa imara katika malezi yake. Kila jambo lina umuhimu wake. Nafasi ya washauri : Hawa wanajumuisha wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zako wanaotumia nafasi walizonazo kwako kukushauri la kufanya. Hawa wana umuhimu sana kwani waliokuzidi umri hukupatia yale yaliyowasaidia kuwa watu wa heshima katika jamii

MAGAZETINI LEO JUMAMOSI OKT 29

Image

Ushirikina chanzo kikuu cha mauaji Kanda ya Ziwa - Askofu Kasalla

Image
USHIRIKINA umetajwa kuwa sababu kubwa ya kukithiri kwa mauaji kwa Kanda ya Ziwa, na kwamba kuamini zaidi katika imani za kishirikina kuliko Mungu kunachochea wimbi hilo la mauaji. Hayo yamebainishwa na Askofu Flavian Kasalla wa Jimbo Katoliki Geita katika ziara yake ya kichungaji aliyoifanya katika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima iliyopo Geita mjini, iliyoambatana na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara kwa waamini 153 wa Parokia hiyo. Askofu Kasala amesema kuwa tabia za kupiga ramli kwa waganga wa kienyeji ambao wengi huishia kuwa wachonganishi, zimekuwa kichocheo kikubwa cha mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu kubwa ya kuuawa na watu wanaodaiwa kutafuta utajiri kwa kukatisha maisha ya wengine. Aidha Askofu Kasalla ameiomba Serikali kuangalia upya Leseni za uganga walizozitoa kwa waganga hao, ambazo zimewapa uhalali wa kupiga ramli na kuhatarisha maisha ya wengine. "Ndugu zangu wapendwa natumia fursa hii kuiomba s

Zakayo, shuka upesi

Image
JACK Higgens ni mwandishi wa riwaya ‘The Eagle Has Landed’ – ‘Tai Ametua’ – aliulizwa ni kitu gani alipendelea kukijua au kukifahamu alipokuwa bado kijana. Jibu likawa, laiti ningejua kwamba ukifika juu, hakuna lo lote pale. Naye mwandishi R. H. Benson anasema kuwa – ukuu wa maisha ya mtu haupo katika sifa zake mbalimbali za nje bali katika majitoleo na sadaka zake. Ndugu wapendwa, tunaona katika somo letu la Injili kuwa katika watu waliokuwa na mafanikio katika mazingira ya wakati wake ni huyu Zakayo ambaye leo tunasikia habari yake katika Injili Takatifu. Kama mtoza ushuru alikuwa kibaraka wa watawala wapagani Warumi. Watoza ushuru walifanya kazi kwa niaba ya hawa watawala. Kwa hiyo walichukiwa kama vibaraka wa wapagani Warumi ambao hawakupendwa na Wayahudi na pia walichukiwa kwa kuwa kodi ilichukiwa na wenyeji. Mbele ya wenyeji walikuwa ni watenda dhambi. Huyu Zakayo alikuwa mtoza ushuru mkuu wa mji wa Yeriko. Kwa kawaida utawala uliweka kiwango cha kodi cha kutoa kwa