CARITAS TANZANIA INAVYOWASAIDIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO

Mara baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi Septemba 10, 2016 Idara ya Caritas Jimbo Katoliki Bukoba ilifanya jitihada za makusudi za kutathmini madhara ya tetemeko hilo na kubaini mahitaji yanayopaswa kupewa kipaumbele.
Katibu wa Caritas Jimbo Katoliki Bukoba Padri Deogratius Mwikira, ameeleza kuwa ofisi yake imefanya tathmini ya kubaini mahitaji ya haraka kwa wahanga wa tetemeko hilo.
Tathmini hiyo ilifanywa na jopo la wana Caritas kwa kuzunguka nakutazama hali halisi, kufanya mahojiano ma viongozi wa vijiji, dini, walimu wakuu na wakuu wa shule, na wawakilishi wa vyama vya ushirika.


Tathmini hiyo imefanyika katika vijiji vya Nyarugongo, Kiilima, karagala, Kigazi, Ruhano, Katolerwa na Minziro. Vijiji vingine ni pamoja na Kabyaile, Katano, Bushaga, Ntungamo, Ibosa, Busimbe B na Bugambakamo.
Tathmini hiyo imebaini uharibifu wa shule 13, majengo ya dini 11, nyumba za watu wasiojiweza 2, Vituo vya afya 3 na vyama vya ushirika vitatu.
Aidha watu waliofanyiwa tathmini hiyo wameonyesha kukosa usalma kwa kuwa wanalala nje, kwenye baridi na mali zao zikiwa nje.
Idadi ya makazi
Idadi ya Kaya katika vijiji 14 vilivyofanyiwa utafiti
5648
Kaya ziazoongozwa na wanawake
538
Kaya zenye walemavu
61
Kaya zinazoongozwa na watoto
91

Mtawanyiko baada ya tetemeko
Wakazi wanaoishi/wahifadhi majirani zao
67
Waliohama makazi yao
495







Msaada mpaka sasa
WALIOTOA
AINA YA MSAADA
ALIYEPOKEA
Serikali
Mablanketi, mashuka, biskuti, mchele, maharage, sukari, ndoo
Walioathirika katika kijiji cha Minziro
Walioguswa
mashuka
Dispensari 1



Mahitaji
Msaada unaohitajika
Wahusika
Mahema
Watoto, wazee, walemavu, wajane
Mablanketi
Watoto, wazee, walemavu, wajane
Mashuka
Watoto, wazee, walemavu, wajane
Saruji
Watoto, wazee, walemavu, wajane
Mabati
Watoto, wazee, walemavu, wajane


MSAADA WA MFUKO WA MSAMARIA MWEMA KWA WALIOATHIRIKA NA TETEMEKO LA ARDHI
Kama ilivyo ada ya Kanisa Katoliki, ifikapo Jumapili ya kwanza ya mwezi Septemba huadhimishwa Jumapili ya Msamaria Mwema. Hapo katika parokia zote na vigango vyote vya Kanisa Katoliki huhamasisha waamini kuchangia vitu na pesa kwa ajili ya watu wahitaji.
Kwa kutambua mahitaji ya wahanga wa tetemeko la ardhi, Idara ya Caritas Bukoba iliamua kugawa mchango uliotolewa katika jumapili ya msamaria mwema kwa waathirika wa tetemeko, kupitia Kamati ya maafa ya mkoa chini ya uongozi wa
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mustafa Kijuu.
Vitu vilivyotolewa ni kama ifuatavyo:
Mashuka pea 100     Tsh 1,500,000
Nguo za watoto          Tsh 93,400
Nguo za kike                 Tsh 1,460,000
Nguo za kiume             Tsh 840, 0000
Viatu                               Tsh 265,000
Madaftari                      Tsh 530,000
Kalamu za wino              Tsh 37,000
Kalamu ya risasi              Tsh 10,000
Sabuni za miche              Tsh 85,000
Sabuni za kuogea            Tsh 6,500
Jumla Kuu                          Tsh 4,734,900




Baada ya tathmini, CARITAS yawafariji waathirika wa tetemeko
 BAADA ya kufanya tathmini ya madhara yaliyoletwa na tetemeko la ardhi lililotokea Septemba 10 mkoani Kagera, Idara ya Caritas katika Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, imewafuta machozi wahanga hao kwa kuwapelekea msaada wa vyakula vilivyosindikwa vyenye thamani ya Tsh. Milioni 108.
Katibu Mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui
Akiongea na Kiongozi ofisi kwake, Katibu Mtendaji wa Caritas Tanzania, Laurent Masui ameeleza kuwa msaada huo wa vyakula vilivyosindikwa, ambavyo ni nyama na maharage, umewasilishwa kwa Idara ya Caritas Jimbo Katoliki Bukoba, kwa ajili ya kupanga utaratibu unaofaa wa kuwafikishia wahanga hao.
“Tumepeleka msaada wa tani 20 za vyakula vilivyosindikwa. Msaada huo utapelekwa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi, na watapewa kulingana na mahitaji yao. Idara ya Caritas Jimbo Katoliki Bukoba itaratibu namna ya kuwafikia walengwa” ameeleza.
Licha ya msaada huo, caritas imeshafanya tathmini ya kuzitambua familia zenye uhitaji maalum ili nao waweze kupatiwa msaada  kadiri ya mahitaji yao. Ametaja familia hizo kuwa ni pamoja na zile za wajane, walemavu ambapo watapatiwa vifaa vya nyumbani na vya ujenzi.



“Tumeshafanya tathmini na kuzitambua familia ambazo hazijiwezi na zenye uhitaji maalum. Tunajipanga ili kupata namna bora ya kuwasaidia vifaa vya ujenzi na vya nyumbani kama vile mabati, mifuko ya saruji, na vyombo vya matumizi ya nyumbani” ameongeza.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU