CSSC KUJENGA ' SOBER HOUSE' JIMBONI TABORA


Tume ya Kikristo ya Kanda ya Magharibi inatarajia kujenga nyumba ya utulivu nje kidogo ya Manispaa ya Tabora hivi karibuni.
Akiongea na Blog hii ofisini kwake mwisho wa wiki meneja wa tume hiyo Elizabeth Lubike alisema Tume hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kuona vijana na watu wazima ambao wameathiriwa na madawa ya kulevya na pombe.
Kituo hicho kitajikita katika kuwarudisha au kuwakarabati watu walioathirika katika mikoa ya Tabora, Kigoma,na Singida.Aidha katika mkutano huo wa siku mmoja wajumbe walizungumzia pia utekelezaji wa mipango ,sera na mikakati ya serikali kupitia tume hiyo (CSSC). 
Mkutano huo pia ulijadili suala ya kutoa ushauri kwa watendaji wa tume hiyo. Meneja Lubike alisema mkutano pia ulijadili Ripoti ya utekelezaji wa mpango kazi wa  mwaka uliopita.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo ni Askofu Mkuu Paulo Ruzoka wa kanisa Katoliki, Askofu Dr.Alex Mkumbo(KKKT), Askofu John Lupaa (ACT DRV), Askofu Elias Chakupewa (Anglican), Askofu Joseph Mlola (Kanisa Katoliki).
Upande wa serikali alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri , pamoja na makatibu wa Afya na Elimu toka mikoa yote inayounda kanda ya Magaribi ndani ya Tume hiyo.
Moja ya maazimio ni kwamba mwakani Tume itakutana mara mbili , pia mkutano huo utahudhuriwa na wakuu wote wa mikoa ya kanda ya Magharibi na wakuu wote wa Wilaya za Mkoa wa Tabora

Pd Thomas Mambo, Tabora

Comments

  1. Mungu ni mwema mradi huyu uwe msingi wa tumaini kwa kundi la vijana ili wamrudie Mungu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU