" TUEPUKE UNAFIKI" PAPA FRANSISKO AONYA

Baba Mtakatifu Fransisko amekemea vikali tabia za unafiki kwa baadhi ya waamini huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha maagizo ya Bwana wetu Yesu Kristo. Ameyasema hayo katika kanisa dogo la Mtakatifu Marta ndani ya Vatican.

Homilia yake ilitafakari kwa kina somo kutoka barua ya Mtume Paulo kwa Wagalatia na pia Injili ya siku ambamo Yesu anakemea unafiki wa mafarisayo, kujifanya kuwa watakatifu kumbe mioyo yao imejaa udhalimu na uovu.

“Ninyi Mafarisayo , huosha kikombe na sahani kwa nje lakini ndani mmejaa udhalimu na uovu”. Yesu aliwaonya kwamba,  aliyetengenza nje  ni huyohuyo pia aliyetengeneza ndani pia. Na hivyo akawahimiza watoe kwa maskiini walivyo navyo na vingine vyote vitakuwa halali kwao".(Luka.11;38-42)

Papa amesisitiza juu ya uhuru wa ndani, uhuru wa kutenda mema bila ya kujionyesha au kujitangaza jambo ambalo limeshamiri katika jamii zetu. Amekumbusha kila muumini atafakari kwa kina na kukumbuka maisha aliyoishi Yesu.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU