MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI


Mt Maria Goreti alizaliwa mwaka 1890,Oktoba 16,huko Corinaldo,Ancona nchini Italia.Baba yake ambaye alikuwa mkulima,aliiamishia familia huko Ferrier di Conca,karibu na Anzio.Akafa baada ya kuugua malaria.Mama yake alifanya kazi nyingi kumudu familia.Wakati mama yake,kaka na dada zake wakienda shambani,yeye aliachwa nyumbani akipika,kusafisha nyumba na kumwangalia mdogo wake aliyeitwa Teresa.Japo familia ilikuwa maskini,lakini bado walimwamini Mungu.
Mwaka 1902,Julai 5,jirani yao aliyeitwa Alessandra,alijaribu kumbaka Mtakatifu Maria Goreti.Maria alipiga yowe na kumwambia mbakaji,Hiyo ni dhambi,Mungu hapendi.Akasema pia kuwa yu tayari kufa kuliko kufanya dhambi ile.Alessandro alitoa kisu,akamchoma Maria mara 14,Sehemu mbalimbali .Hakupata msaada wowote mpaka mama yake,na ndugu zake waliporudi kutoka shamba.Wakampeleka hospitali ambako alifanyiwa matibabu na kushonwa bila ganzi.Daktari alikuwa na hakika kuwa Maria angekufa.Alimwomba Maria akienda mbinguni asimsahau.Siku iliyofuata alisema kuwa,amemsamehe Alessandro na angependa akutane nae mbinguni.
Mt Maria Goreti alikufa siku  hiyo tarehe Julai 6 1902,akiangalia picha ya Bikira Maria,na akiwa ameshika msalaba kifuani mwake.Baada ya familia ya Mtakatifu Maria kujua,Alessandro alikamatwa na kuhojiwa.Alikiri kujaribu kubaka,na akathibitisha kuwa hakufanikiwa kumbaka.Alessandro akahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.Akiwa jela aliota kuwa alikuwa bustanini,Maria akampa ua.Alipolipokea lilimuunguza katika viganja vyake.Alivyoamka alibadilika ,akawa mpya.Alitubu dhambi yake,akaishi maisha mapya.Akakaa jela miaka 27,alipoachiwa alienda moja kwa Moja kwa Mama yake Maria,akamwomba msamaha.Mama huyo alisema,Mwanangu alikusamehe,mimi siwezi kukukatalia msamaha.
Mtakatifu Maria GoretiAlitangazwa mwenyeheri mwaka  1947,April 27 na Papa Pius XII.Akatangazwa mtakatifu mwaka 1950, Juni 24.

Watakatifu wengine wa leo ni

Mt. Abrahamites Monks
Mt. Dominica
Mt. Goar
Mashahidi wa Abrahamites
Mt. Merryn
Mt. Modwenna
Mt. Monennaa
Bl. Nazaria Ignacia March Mesa
Mt. Noyala
Mt. Rixius Varus
Mt. Romulus na wenzake
Mt. Sexburga
Bl. Thomas Alfield
Mt. Tranquillinus

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU