TV TUMAINI KUONEKANA NCHI NZIMA

Mpango Mtakatifu wa kuwezesha TV Tumaini ionekane kwa waamini wakatoliki wote nchini umekaribia kukamilika.Hii inafuatia kuundwa kikosi kazi makini ambacho pamoja na mambo mengine kimepewa jukumu la kufanya uhamasishaji mkubwa katika majimbo yote 34.Mpango huu unatarajia ndani ya kipindi cha miezi 6 TV Tumaini iwe inaonekana pote nchini na baadhi ya nchi jirani.TV Tumaini itaonekana katika SATELITE kupitia kampuni ya SIMBA NET na kuwa chombo bora cha uinjilishaji.Mpango huo utakaokuwa chini ya Baraza la Maaskofu kitasimamia uhamasishaji,uelimishaji wa waamini,kusimamia taratibu mbalimbali na kufanikisha jukumu hilo.Hata hivyo ili kufikia mafanikio hayo michango kutoka majimboni inahitajika,tamasha la uhamasishaji litafanyika hivi karibuni,wahisani pamoja na mbinu zingine.TV Tumaini inayomilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki na kuendeshwa chini ya uangalizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam kwa sasa inaonekana katika baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam.

Na Bernard James..Mkurugenzi wa Mawasiliano Baraza la Maaskofu Katoliki








Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU