IFAHAMU JUMAPILI YA BAHARI(10 Julai 2016)
Jumapili ya bahari
- Jumapili hii inaadhimishwa kila Jumapili ya pili ya mwezi wa saba. Kanisa linawaalika na kujumuika na waumini wote ulimwenguni, kuwaombea wote wale wanaohusika, na kufanya kazi katika mazingira ya bahari, maziwa na mito. Kanisa linamshukuru Mungu kwa uwepo wa mabaharia na wavuvi linawashukuru mabaharia kwa kazi zao na kuwaombea waweze kuwa na uvumulivu, na ujasiri katika upweke wao na magumu yote wanayokumbana nayo, waendelee kuimarika kiimani na katika wajibu wao. Zaidi ya asilima 90 ya biashara za aina zote, za kimataifa zinapitia baharini.
- Kanisa linawatambua, linajali na kuheshimu mabaharia, wavuvi na familia zao, linakiri mchango wao mkubwa katika kurahisisha na kufanikisha shughuli mbalimbali za kijamii. Kwa njia ya bidhaa wanazosarifisha wao ni kiungo cha biashara za kitaifa na kimataifa. Kanisa linatambua magumu wanayoyapata katika makazi na masilahi yao linawafikiria, linawakumbuka katika kuwaombea ili wazidi kudumu katika kazi zao.
- Kuwatia moyo wote wale wenye “wito” na uelekeo wa ubaharia na uvuvi kwani bado ni muhimu na wanahitajika.
- Kuwaombea Mungu awalaze mahali pema mabaharia, wavuvi, famila zao na wale wote ambao wamepoteza maisha yao baharini, au ziwani, au kwenye mito, wakiwa kazini, au wasafiri. Yapo maeneo ambapo jumapili hii huadhimishwa ufukweni, na wakati wa kuwaombea kama ishara ya kuwakumbuka, mashada ya maua yanatupwa baharini.
- Kipindi ambacho kwa njia ya jumuiya za utume wa bahari, waumini wanahamasishwa kupanga, kukuza na kuboresha huduma na misaada itolewayo na jumuiya za kikristu wa mahali walipo mabaharia na wavuvi. Wanakumbushwa kuwa na moyo wa ukarimu, upendo, mshikamano na kuwatendea mema.
- Bahari inabadilisha sana maisha ya mabaharia na wavuvi. Taratibu za maisha yao huratibiwa na shughuli na mazingira ya bahari, au ziwani, au mito mikubwa wanamofanya kazi. Mara nyingi wanakutana na hali za upweke, na pia mbali na familia zao.
- Baadhi ya mabaharia na wavuvi wanaishi katika mazingira magumu, duni ya hatari na yenye kipato kidogo, wengine wanajikuta katika masharti na mazingira magumu ya kazi
Huduma maalumu au za kipekee zinatolewa na kanisa kwa ajili
yao ili waweze kujisikia ni wanajumuiya na kuwa utu na kazi zao unatambulika
kuheshimiwa na kutegemezwa.
- Kuwapokea kwa ukarimu, undugu na kuwatendea mema, wafikapo kwenye vituo vya mabaharia. Mfano. Mission to seafarers and Stella Maris Centres. Vituo vya utume wa bahari vina huduma zifuatazo: Eneo la ibaada, sala (Kanisa) viburudisho, chakula kuogelea, mawasiliano. simu na interent.
- Wahudumu wa utume wa bahari kupitia kwa mlezi, chaplain, kushirikiana na viongozi wa bahari ili kufahamu meli zinazoingia.
- Kuwa na utaratibu wa kuwatembelea mabaharia melini mara wafikapo. Kuwapatia huduma za kiroho au melini au kwenye vituo vya utume wa bahari, kulingana na mahitaji yao.
- Kuwasaidia wawapo na shida mbalimbali kama afya, na maswala ya haki za binadamu, kwa kuwasiliana na mashirika husika
- Kuwafikiria, kuwakumbuka, kuwaombea mabaharia na wavuvi katika sala. Kanisa limeweka siku/pekee maalumu Jumapili ya bahari kwa ajili ya kuwaombea.
WASIMAMIZI WA UTUME WA BAHARI
1.
Mama Bikira Maria ;-Vituo vya utume wa
bahari vinajulikana kwa jina STELLA MARIS (Nyota ya Bahari)
Ulimwengu wa bahari unamtambua kama mwombezi na msimamizi wao.
2. -Watakatifu Petro na Andrea - wote wavuvi
3. -Mt Francis wa Paola (1416-1517) -
Msimamizi wa mabaharia wa Italia.
4. -Mt. Nicolaus – askofu wa myra. Tangu karne ya tatu
anatambulikana kama msimamizi wa wahudumu wa mitumbwi.
5. Lukas Banabakintu.
Mmoja wa mashahidi 22 wa Uganda.
MAJIMBO
YANAYOHUSIANISHWA NA UTUME WA BAHARI NA MAZIWA –TANZANIA
1.
Jimbo kuu la Dar-es-Salaam,Majimbo ya
Mtwara,Lindi,Tanga na Zanzibar
2.
Majimbo eneo la
maziwa makuu;-Mbinga,Njombe,Mbeya,
Sumbawanga,Kigoma,Rulenge,GeitaMusoma,Shinyanga,Jimbo kuu la Mwanza.
3.
Majimbo eneo la
mabwawa na mito mikubwa;- Same,Kilimanjaro ,Iringa nk
Comments
Post a Comment