MKOMBOZI BENKI HIYOOO MOROGORO

Benki ya Mkombozi imefungua tawi lake Jimboni Morogoro ikiwa ni katika kuhakikisha inawafikia watumiaji wengi zaidi na kwa huduma bora na za kisasa kabisa.Akizindua tawi hilo,Askofu wa Jimbo Katoliki Morogoro Telesphor Mkude amewataka watumiaji wa huduma hiyo kuitumia fursa hiyo adimu.Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro Dokta Steven Kebwe pia amesema ni wakati muafaka kwa wana Morogoro kupata huduma bora za kibenki na kuwasihi kuchangamkia huduma hiyo waliyosogezewa.Tawi hilo lipo katika jengo la kitega uchumi cha Jimbo Katoliki Morogoro kilichozinduliwa hivi karibuni(Habari na Bernard James,Picha kwa hisani ya ITV)










Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU