"MKRISTO MAANA YAKE KUHUBIRI INJILI"PAPA FRANCIS


(Vatican Radio) Jumapili kabla ya sala ya Malaika wa Bwana , Papa Francisko aliasa kwamba, kuwa Mkristo maana yake ni kumwakilishi Kristo. Papa alitoa wito huo kwa mahujaji na wageni waliokuwa wamekusanyika katika uwanja wa Kanisa Kuu la  Mtakatifu Petro mjini Vatican akitafakari juu ya njia mbalimbali ambazo Wakristo wa kila umri, kila hali,  jinsi wanavyoweza kutoa jibu  la  kawaida kama Wabatizwa, katika utume wa Kanisa, wakiwa  kama  mmisionari - Mabalozi wa Kristo,  katika maisha ya kila siku, kwa watu karibu na mbali.
Papa alihoji , ni kwa  roho yupi, mfuasi wa Yesu  anaweza  kutekeleza ujumbe huu? Na alitoa jibu lake akisema  kuwa,  awali ya  yote, Mkristo ni lazima kufahamu hali halisi kwamba , utume huu ni mgumu kwa maana ni kutenda kinyume na  kazi za shetani . Na hivyo Mtumishi wa Injili ni lazima ajue wazi kwamba, ni kwenda kinyume na kila aina ya vishawishi vya kidunia. Ndiyo maana Yesu alisema,  “ninawatumeni  kama kondoo  kati ya  mbwa mwitu “.
Baba Mtakatifu  Francisko aliendelea kueleza kwamba, kumbe, uhasama ulikuwepo muda wote tangu mwanzo wa Ukristo.  Yesu alitambua hilo, ndiyo maana aliwaonya wanafunzi wake wa kwanza kuwa,  kuitumikia Injili ni kutenda kinyume na kazi ya yule Mwovu. Kuitumia  Injili ni lazima kujitahidi kujiweka huru dhidi ya dhambi zote. Ndyo maana alisema, , msibebe mfuko, wala mkoba, wala viatu – maana yake ni kutotegemea nguvu yoyote ya kibinadamu isipokuwa  kutegemea  nguvu ya msalaba wa Kristo.
Papa Francis aliendelea kufafanua kuwa  kuacha kutegemea nguvu zote za kibindamu ina maana ya kupuuza vishawishi na uwezo wote wa nguvu binafsi, na hivyo kuwa mtumishi mnyenyekevu wa Injli , katika kupitia utume wa kazi za  kanisa za kumkomboa binadamu, zinazofanikishwa na Yesu mwenyewe aliyejitoa kuwa  sadaka ya wokovu katika kifo chake cha msalabani kwa ajili ya kumkomboa binadamu. Kwa kufanya hivyo , Papa alisema , moyo wa mtu hujazwa na furaha ya kweli.
Papa alieleza na kutaja kwa  jinsi gani Kanisa hufurahia kuona watu wanasikiliza wito huu wa  Kanisa, kupokea Habari njema kupitia njia ya majitolea ya watu wengi , wanawake na wanaume , ambao kila siku huitangaza injili wakiwa ni Maaskofu , Mapadre, watawa, watu  walioweka maisha yao wakfu, wamisionari wa wanawake na wanaume, wenye kutoa mwaliko huu , unaowafikia vijana wengi  kama ilivyokuwa kuwa kwa wakati huo katika Uwanja huu wa Kanisa Kuu la Mtakatifu. Papa aliwahimiza wote wasikilize kwa  makini wito wa Bwana unaowataka wafuatane nae.
Aliwasihi wasiogope kufuatana na Yesu, badala yake wawe na ujasiri na kuwaleta wengine wengi zaidi kwa mwanga wa  juhudi za kitume, zilizoonyeshwa na mifano mingi ya wafuasi wa Yesu. Baada ya ufafanuzi na sala ya Malaika wa Bwana , Papa alitoa baraka zake za kitume kwa wote waliofika kumsikiliza. 

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI