MAHAKAMA YA MAFISADI:MAJENGO KUKABIDHIWA JUMATATU
WAKATI
Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati
wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa kukabidhiwa keshokutwa
jumatatu.
Jaji
Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema jana kuwa mkandarasi
aliyekabidhiwa kazi ya kukarabati majengo hayo yaliyopo katika Shule Kuu
ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi cha Simu 2000, Ubungo Dar es
Salaam, yako katika hatua za mwisho za ukarabati.
Akizungumza
katika viwanja vya Karimjee baada ya kuapisha mawakili wapya 623 wa
Mahakama Kuu, Jaji Chande alisema tayari Bunge limeshapitisha muswada wa
sheria ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.
Alisema
kwa sasa muswada huo utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa ajili ya kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria hiyo
itatangazwa katika gazeti la Serikali ili kuruhusu shughuli za mahakama
hiyo kuanza.
Kwa
mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko tayari kuendesha Divisheni hiyo ya
Mahakama na baada ya kukabidhiwa majengo hayo, wataanza kutoa semina kwa
majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo
itakavyoendesha shughuli zake.
Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.
Comments
Post a Comment