Posts

Showing posts with the label liturujia

KUELEKEA KILELE CHA JUBILEI KUU – ARI YA KICHUNGAJI MUHIMU

Image
K atika kuadhimisha Jubilei ya miaka mia moja na hamsini ya Uinjilishaji, Kanisa Katoliki Tanzania linamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwatuma Wamisionari kuja kutangaza Injili Tanzania. Kwa kuzingatia jinsi Wamisionari walivyojitoa katika kutangaza Injili, na kupambana na changamoto mbalimbali, Kanisa la Tanzania linapaswa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa Uinjilishaji wa miaka hiyo mia na hamsini. Awamu za Uinjilishaji Wataalamu wa historia hutueleza kwamba katika Afrika ya Mashariki, Uinjilishaji wa kwanza ulifanywa na Wamisionari wa shirika la Mtakatifu Agustino mnamo mwishoni mwa karne ya kumi na tano. Wamisionari hao walifuatana na mvumbuzi mashuhuri aitwaye Vasco da Gama, na walifika Zanzibari 1499 na lengo lake lilikuwa kutafuta njia ya kwenda India na mashariki ya mbali. Katika kuinjilisha, wamisionari hao walipata upinzani mkubwa kutoka kwa Waarabu.   Walijitahidi kuendelea lakini mnamo mwaka 1698 Uinjilishaji huo ni kama ulififia. Sababu kubwa ya...

KALENDA YA LITURUJIA NI KWA AJILI YA WAKRISTO WOTE

Image
Kalenda ya Liturujia ni kwa ajili ya Mapadri na watawa? La, hasha! Hiyo siyo kweli. Kalenda ya Liturujia inaandaliwa ili kila Mkristo aweze kuitumia. Kalenda ya Liturujia ni kwa ajili ya kutumia Wakristo wote wakatoliki. Kalenda ya Liturujia Kalenda ya Liturujia ni mwongozo wa kiliturujia ambao hutolewa na Idara ya Baba Mtakatifu huko Vatikano – Roma, Idara inayosimamia Liturujia Takatifu; mwongozo huo unawekwa katika lugha ya Kiswahili na Idara ya Liturujia ili kuwawezesha Wakristo wakatoliki nchini waweze kutumia. Kalenda hiyo     huandaliwa kila mwaka kwa ajili ya Maadhimisho ya Misa na kwa ajili ya kusali Sala ya Kanisa. Kalenda ya Liturujia siyo ya kutundikwa ukutani, bali inaandikwa kwa mtindo wa kijitabu kidogo chenye kurasa takriban 150 ili kwamba Mkristo akishajipatia anaweza kuiweka mfukoni na kusafiri nayo kwa urahisi. Kwa kuwa inatoa mwongozo wa kuadhimisha Misa na kusali Sala ya Kanisa, baadhi ya waamini wamekuwa na fikra kwamba inatengenezwa kwa ajili ...

Shukuru usikufuru

INGAWA tuna mioyo midogo lakini inaweza kubeba jambo kubwa nalo ni shukrani. “Tunapotoa kwa furaha na kupokea kwa shukrani, kila mtu anabarikiwa,” alisema Maya Angelou.   Kuna methali isemayo, “Asiyeshukuru kwa jambo dago apewalo hatashukuru kwa jambo kubwa.” Leo hii wakatoliki sehemu zote duniani wanaandamana kusherehekea sherehe inayojulikana kama “Mwili na Damu ya Kristo.” Kwa jina lingine sherehe hii inajulikana kama “Sherehe ya Ekaristi Takatifu.” Neno “Ekaristi” linatokana na neno la Kigiriki ambalo linamaanisha shukrani. Ni sherehe inayohusu kumshukuru Mungu na utamaduni wa kushukuru. Kushukuru ni kitovu cha sherehe hii. Shukuru kwa kila jambo. Sherehe ya Leo ya wakatoliki inahusu utamaduni wa kushukuru. Waluhya wana methali isemayo, “Nyama choma haiwezi kuwa tamu ukamsahau aliyeichoma.” Methali hii inakazia kuwa na utamaduni wa kushukuru. Kama umepewa siyo siri. Watu wanaona jinsi Mungu alivyokubariki na hivyo kwa mantiki hii wakatoliki wanaandamana had...