MUSOMA WAPATA VIONGOZI HALMASHAURI YA WALEI
Picha
ya pamoja wajumbe wa Halmashauri ya Walei Jimbo katoliki Musoma
walioshiriki uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya, uchaguzi uliosimamiwa
na Mwenyekiti
wa Halmashauri kutoka Taifa Ndugu Gasper Mathew Makululi na Alvera Kabwogi ambaye ni mtunza hazina wa Halmashauri ya Walei Taifa uliofanyika katika ukumbi wa Conference Centre
Jimbo la Musoma hivi karibuni(picha na Veronica Modest)
Naibu Askofu wa Jimbo katoliki Musoma na msimamizi wa uchaguzi Padri Julius Ogolla (katikati) akiwatizama Mwenyekiti
wa Halmashauri kutoka Taifa Ndugu Gasper Mathew Makululi kutoka
jimbo katoliki Moshi (kushoto) na
Alvera Kabwogi ambaye ni mtunza hazina wa Halmashauri ya Walei Taifa
kutoka
Jimbo kuu katoliki Dar Es Salaam(kulia) wakihesabu karatasi za kura katika uchaguzi
wa kuwapata viongozi uliofanyika katika ukumbi wa Conference Centre
Jimbo la Musoma, hivi karibuni(picha na Veronica Modest)
Picha ya pamoja Naibu Askofu wa Jimbo katoliki Musoma Padri Julius Ogolla, Mwenyekiti
wa Halmashauri kutoka Taifa Ndugu Gasper Mathew Makululi kutoka
jimbo katoliki Moshi na
Alvera Kabwogi ambaye ni mtunza hazina wa Halmashauri ya Walei Taifa
kutoka
Jimbo kuu katoliki Dar Es Salaam baada ya kumaliza uchaguzi uliofanyika katika ukumbi wa Conference Centre
Jimbo la Musoma,Hivi karibuni(picha na Veronica Modest)
Veronica Modest ,Musoma.
Halmashauri ya Walei Jimbo katoliki Musoma imepata viongozi wapya ambao wataongoza kwa
kipindi cha miaka mitatu kuanzia 2016 hadi 2019 , katika mkutano wa uchaguzi huo uliofanyika Oktoba 1, mwaka huu katika
ukumbi wa Conference centre uliopo Jimboni Musoma .
Kabla ya uchaguzi huo, wajumbe wa mkutano huo wakiongozwa na viongozi kutoka Halmashauri ya Walei Taifa, walianza kwa semina ya siku moja wakijifunza juu ya umuhimu wa kutenga fungu
la kumi, semina iliyoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kutoka Taifa
Ndugu Gasper Mathew Makululi kwa kushirikiana na Alvera Kabwogi ambaye ni mtunza hazina wa
Halmashauri ya Walei Taifa.
Baada ya semina hiyo yalifuata mafungo kwa ajili ya kumuomba
Mwenyezi Mungu aweze kuwasaidia wapate viongozi bora watakaolitumikia kanisa na
Jimbo kwa uaminifu, na uchaguzi huo
ulisimamiwa na viongozi wa Kitaifa pamoja na Naibu Askofu wa Jimbo la Musoma Padri
Julius Ogolla na kubahatika kuwapata
viongozi watakaowaongoza katika kipindi
hicho.
Viongozi waliochaguliwa ni Raymond Nyamasagi -Mwenyekiti kutoka parokia
ya Mugumu, Alex Malima Kisurura -Makamu Mwenyekiti kutoka Parokia ya Musoma
Mjini, Richard Getenyi - Katibu kutoka Parokia ya Nyamiongo, Julius Magige - Katibu Msaidizi kutoka Parokia ya Tarime na
Joseph Getunguye – Mweka hazina Kutoka parokia ya Mugumu
Akizungumza mara baada ya uchaguzi, Mwenyekiti Mpya wa
Halmashauri hiyo Raymond Nyamasagi aliwashukuru sana wajumbe hao kwa kumpatia
viongozi ambao watashirikiana katika kufikia malengo ya Halmashauri hiyo, sambamba
na kuwahamasisha wajumbe wote walioshiriki kuhakikisha kile walichojifunza
wanakwenda kuwafunza waamini wao ili kuonyesha muungano mzuri ndani ya Kanisa.
Kwa upande wake katibu ambaye ndiye msimamizi mkuu wa
shughuli za halmashauri hiyo ndugu Richard Getenyi aliwaomba wajumbe kupitia parokia zao kuhakikisha wanajitahidi kushiriki
kikamilifu, ili kuweza kusaidia katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kila siku pamoja na kulipa michango mbalimbali mapema kwa ajili ya mkutano mkuu wa
kitaifa.
Baada ya uchaguzi huo viongozi hao wakiongozana na wajumbe
wa mkutano huo walishiriki ibada ya kuwabariki viongozi hao ,ambayo iliongozwa
na Paroko wa Makutano Padri Julius Ogolla.
Comments
Post a Comment