Afya ya Baba Mtakatifu Fransisko inaimarika


DR. Matteo Bruni Msemaji Mkuu wa Vatikani katika taarifa yake kwa vyombo vya habari amebainisha kwamba, afya ya Baba Mtakatifu Fransisko  ambaye hivi karibuni alikumbwa na mafua makali inaimarika.
Hivi karibuni Papa Fransisko alikumbwa na mafua makali ambayo yalimsababisha ashindwe kuhudhuria Mafungo ya Kwaresima 2020 kwa wasaidizi wa karibu wa Baba Mtakatifu, “Curia Romana” kuanzia Machi 1- 6 mwaka 2020 huko Ariccia nje kidogo ya mji wa Roma.
Kwa sasa Papa Fransisko anaendelea pia kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwenye Kikanisa cha Mtakatifu Martha kilichoko mjini Vatikani.
Baba Mtakatifu pia anaendelea kufuatilia tafakari za mafungo ya Kwaresima zinazotolewa kwa wafanyakazi wa “Curia Romana” huko Ariccia, nje kidogo ya mji wa Roma.
Dr. Matteo Bruni amefafanua kwamba, Baba Mtakatifu anasumbuliwa na mafua ambayo hayana uhusiano wowote na magonjwa mengine.
Tafakari wakati wa mafungo inaongozwa na Padri Pietro Enrico Bovati, SJ, Katibu Mkuu wa Tume ya Kipapa ya Biblia na Mtaalam wa Sayansi ya Maandiko Mtakatifu.
Kauli mbiu ya mafungo hayo ni “Kile kijiti kiliwaka moto: mkutano kati ya Mwenyezi Mungu na binadamu mintarafu mwanga wa Kitabu cha Kutoka, Injili ya Mathayo na Sala ya Zaburi.”


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU