Maaskofu, mapadri, watakiwa kuhamasisha waamini kushiriki Kongamano la Ekaristi Takatifu


MAjimbo ya Kanda (metropolitani) ya Magharibi yaaswa kuhamasisha zaidi waamini wao kwa namna ya pekee kwenye maandalizi ya Kongamano la nne la Ekaristi Takatifu kitaifa litakofanyika katika Jimbo Kuu Katoliki Tabora.
Rai hiyo imetolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora Mhashamu Paul Ruzoka hivi karibuni katika kikao cha saba cha maandalizi ya Kongamano hilo kilichohudhuriwa na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) Mhashamu Gervas Nyaisonga ambaye  ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki  Mbeya.
Akizungumza katika kikao hicho Askofu Ruzoka amewaomba wajumbe kutoka majimbo ya Tabora, Kahama, Kigoma na Mpanda kuwa mabalozi wa kuhamasisha waamini juu ya tukio hilo muhimu litakatolofanykika 1-5 July mwaka huu.
Aidha amewakumbusha wajumbe kusali sala maalum katika majimbo  yote ya Tanzania  kuliombea Kongamano hilo. Vile vile ameagiza Kurugezi ya Mawasiliano ya Baraza la Maaskofu Tanzania ihakikishe kwamba vyombo vya habari vya majimbo yote vinashirikishwa kikamilifu katika maandalizi na Kongamano lenyewe.
Akitoa salamu za Baraza la Maaskofu Tanzania ,Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga amesema, “Baraza limeridhika na maandalizi ya Kongamano na likotayari kutoa ushirikiano wa hali na mali hadi kufikia kilele cha maadhimisho.”
Pamoja na hayo amewataka wawakilishi wa majimbo ya Metropolitani ya Magharibi kuhamasisha maandalizi na ushiriki kwenye kilele cha Kongamano.
Mada zinazotarajiwa kutolewa kwa washiriki ni; Ekaristi Takatifu na Wahudumu katika historia ya Kanisa, Ekaristi Takatifu katika Maandiko Matakatifu, Ekaristi Takatifu na Umisionari, Ufafanunuzi wa Nembo ya Ekaristi na Mama Bikira Maria na Ekaristi Takatifu.
Aidha kamati ratibishi ya Ekaristi Takatifu ilioneshwa na kuhimizwa kusambaza vitenge vya Kongamano ambavyo vimeandaliwa na Kurungenzi ya Mawasiliano ya Baraza kwa waamini ili kuendelea kulitangaza kongamano kwa waamini.
Ili kufanikisha Kongamano hilo kamati mbalimbali za maandalizi zimekwisha undwa na kupewa majukumu yake.
Aidha Majimbo ya metropolitani ya Magharibi inaendelea na uandishi wa kitabu cha historia ya Ukristo Kanda ya Magaribi, yaani Tabora, Kahama, Kigoma, Mpanda.
Ambayo historia itahusisha majimbo yalikuwa sehemu ya Metropolitani ya Magharibi.
Sambamba na maadalizi hayo kila jimbo la Metropolitani ya Magharibi linaendelea kuratibu mashindano ya kwaya kuanzia ngazi ya kigango mpaka jimbo, ili hapo baadaye kwaya zitakazokuwa zimeshinda katika ngazi ya jimbo zitaletwa kushindana katika ngazi ya metropolitani.
Wakichangia gharama za ushiriki kwa kila muumini, iliamuliwa kila mshiriki atachangia kiasi cha shilingi laki mbili tu za kitanzania , ikiwa ni gharama ya malazi, usafiri wa ndani kuelekea kituo cha hija (Ifucha) na chakula kwa siku zote tano.
Miongoni wa wageni walioshiriki kwenye mkutano huo ni Askofu Edward Mapunda wa Jimbo Katoliki Singida, Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano wa Baraza la Maaskofu Tanzania Mh.Padri Chesco Msaga na Paroko wa Parokia Makongolosi Pd.Gaspar Mwangoka.
Baada ya Mkutano wajumbe walipata fursa ya kutembelea kituo cha Hija cha Jimbo Kuu  Tabora kilicho chini ya watakatifu Yohana Paul II na Terezia wa Calcuta –Ifucha na kuona maendelea ya ujenzi ikiwa na mahali ambapo kilele cha madhimisho ya Kongamano la Ekaristi kitafanyika.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU