Padri awakumbusha waamini umuhimu wa kupokea Ekaristi
Waamini
wenye sifa za kukomunika nchini wametakiwa kuacha tabia ya kukaa bila kushiriki
kula mwili wa Kristo mara wanaposhiriki ibada mbalimbali..
Akizungumza katika mahubiri kwenye ibada ya
Misa takatifu Kigangoni Mbutu, Paroko wa parokia ya Kimbiji Padri Askecher
Luciano amesikitishwa na idadi ndogo ya wakristo wanaojitokeza kushiriki
kupokea Ekaristi Takatifu.
Amesema
kupokea Ekaristi Takatifu ni kula mwili wa Yesu mwenyewe aliyewaamuru waamini
kushiriki fumbo hili.
“Yesu
mwenyewe baada ya kufa na kufufuka aliwatokea vijana wawili waliokuwa
wanazungumza habari zake, kisha naye aliwafumba macho wasimjue na baadaye
walimtambua katika kuumega mkate,” amesema padri Luciano.
Aidha
amewaasa waamini wakristo kutokuogopa kuungama na kwamba amri ya Kanisa
inayosema ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka haimfanyi Mkristo
kuungama mwaka mzima mara moja bali kila itakapobainika kuwa kuna baya au
dhambi imetendeka.
Wakati wa
Kwaresima imeshuhudiwa mapadri kwenye baadhi ya Parokia wakipokea idadi ndogo
ya waaamini waliokwenda kuungama, tofauti na idadi kamili ya wakristo sehemu
husika.
Comments
Post a Comment