‘Elimu inayochochea ukandamizaji haitufai’





ASKOFU wa Jimbo Katoliki Musoma Mhashamu Michael Msonganzila amewakumbusha wahitimu wa kidato cha Sita  kuhakikisha elimu waliyoipata inaleta mabadiliko chanya, hasa katika kupambana na  mila zinazomkandamiza mtoto wa kike na ukatili wa kijinsia kwa ujumla.
Askofu huyo ameyasema hayo hivi karibuni kwenye mahafari ya 15 ya kidato cha sita yaliyofanyika katika ukumbi wa Mwembeni Sekondari ambapo jumla wa wanafunzi 57 wamehitimu kidato cha sita katika shule hiyo na wameanza mitihani yao ya kumaliza Mei 2 mwaka huu.
Amesema kuwa jamii wanayokwenda kuishi nayo imekuwa na vitendo vingi vya kikatili hasa kwa watoto wa kike, lakini kupitia elimu yao waliyoipata shuleni basi wajitahidi kuhakikisha wanaitumia vyema hasa kwa kubadilisha mtazamo wa mila kandamizi na zilizopitwa na wakati, ambazo bado zinaendelea kuleta ubaguzi na ukandamizaji na hata kudhalilisha utu wa mwanadamu ambao ni kinyume kabisa na mpango wa Mungu.
 Ameongeza kuwa katika mafundisho ambayo wameyapata shuleni hapo ya kiroho ya kielimu wanaweza kutumia fursa hiyo katika kuhakikisha jamii inaondokana kabisa na mtazamo hasi juu ya umuhimu wa elimu kwa jinsia zote awe mtoto wa kike au wa kiume kwa kuwa wote wameumbwa na Mungu na wana uwezo sawa wa kufanya vizuri katika masomo yao na hivyo kuleta mafaniko makubwa katika jamii mzima.
 Amewaasa pia wahitimu hao kujiepusha kabisa na matumizi ya dawa za kulenya kwani vijana wengi wanapomaliza elimu yao wamekuwa wakijikuta hawana kitu cha kufanya na hatimaye kujiingiza katika mambo ambayo hayampendezi Mwenyezi Mungu kama vile kutumia dawa za kulevya ambazo serikali ya awamu ya tano inaendelea kupambana nazo,ili kujenga Taifa bora.
 Amewakumbusha pia wazazi na walezi kuhakikisha wanakuwa bega kwa began a watoto hao hasa katika kuangalia mienendo yao na kuwapatia elimu juu ya madhara ya dawa za kulevya na namna ya kuepukana nayo kwakuwa muda mwingi watakuwa nao nyumbani kabla ya kuendelea na hatua nyingine.


Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU