Maaskofu Kanisa Katoliki Kanda ya Magharibi wapiga kambi jimboni Sumbawanga.
Maaskofu wa Kanisa Katoliki Kanda ya Magharibi wamepiga kambi ya siku tano jimboni
Sumbawanga kwa ajili ya kujadili mipango ya kichungaji na maendeleo ya utume
katika kanisa Katoliki Kanda ya Magharibi .
Wakiongoza
na mwenyeji wao Mhashamu Askofu Damian Kyaruzi wa Jimbo Katoliki la Sumbawanga,
wengine ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Tabora Mhashamu Askofu Paul Ruzoka na
Askofu Gervasi Nyaisonga wa Jimbo Katoliki Mpanda. Wengine ni Askofu Joseph Mlola wa Jimbo Katoliki Kigoma na Askofu Rudovik Minde wa Jimbo Katoliki Kahama ambayo inajumuisha majimbo matano likiwemo Jimbo Kuu Tabora.
Akiwapokea
maaskofu hao, mwenyeji wao Askofu wa Jimbo Katoliki Sumbawanga Mhashamu
Damian Kyaruzi amesema kuwa maaskofu hao wanakutana metropolitan ya Tabora
ambapo waliazimia kuwa kila mwaka kwa pamoja watakua wakizungukia majimbo yote
kwa lengo la kufanya mikutano yao na kufanya shughuli za kichungaji katika majimbo
na maazimio hayo yanaanzia katika Jimbo Sumbawanga kuanzia tarehe 25 May hadi
tarehe 29 Mei mwaka huu.
Wakiwa jimboni sumbawanga maaskofu hao
wanatarajia kuwa na mkutano wa maaskofu wa kanda katika kumbi za uaskofuni
pamoja na kutoa kipaimara katika parokia za Kristo mfalme, parokia ya kanisa
kuu, parokia ya Familia Takatifu na katika seminari ndogo ya kaengesa
Akitoa
Baraka kwa waamini wa Jimbo Sumbawanga mara
baada ya mapokezi Askofu Mkuu wa Kanda ya Magharibi Mhashamu Paul Ruzoka
amewashukuru waamini wa Jimbo Sumbawanga kwa mapokezi na kuwaomba wadumu
katika sala na daima na kusimama imara
katika imani ya Kristo mfufuka hasa kwa kipindi hiki cha kuhitimisha kipindi
cha Pasaka.
Na
Emanuel Mayunga Sumbawanga
Comments
Post a Comment