Miaka 150 ya ukristo ilivyomuinua mwanamke Tz

WAKATI Kanisa Katoliki nchini likiadhimisha Yubilei ya miaka 150 ya ukristo Tanzania Bara, imebainika kuwa kanisa limeshiriki kwa kiasi kikubwa katika harakati za kumuinua mwanamke kwa kumpatia nyenzo muhimu ikiwa ni pamoja na elimu, ujuzi na mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Akiongea na Kiongozi ofisini kwake hivi karibuni Mratibu Msaidizi katika Dawati la Jinsia na Maendeleo kupitia Idara ya Caritas Bi. Annesifa John, ameeleza kuwa Caritas imeweza kustawisha na kuinua maisha ya mwanamke Tanzania kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali iliyolenga kumkomboa mwanamke kiuchumi, usaidizi wa kisheria, kisaikolojia, kijamii na kiroho.
Aidha amesema kuwa Caritas, iliyo chini ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), imewezesha upatikanaji wa elimu iliyosaidia kupungua kwa vitendo vya kudharauliwa kwa mwanamke, kunyimwa haki na kuwa nyuma kiuchumi.
“Tumetekeleza miradi mbalimbali hapa nchini iliyolenga kumuinua mwanamke ikiwa ni pamoja na Vikoba, ambapo kupitia miradi hiyo wanawake wameweza kujenga nyumba, kupeleka watoto shule, na kupunguza unyanyasaji wa kijinsia. Tumefanikisha miradi mbalimbali iliyolenga kuwaongezea kipato wanawake kwa kuwawezesha kuendesha miradi ya ufugaji wa kuku, ufundi wa kushona na hata bustani” ameeleza Annesifa.
Akielezea namna ofisi yake ilivyowasaidia wanawake kisheria, Bi Annesifa amesema kuwa Caritas inatekeleza mpango wa usaidizi wa kisheria katika majimbo katoliki yote 34 nchini, na kwamba katika kila kijiji wanachaguliwa watu 25 kisha kujengewa uwezo juu ya masuala ya kisheria ambao huwa msaada kwa wenzao.
“Tunawafundisha maana ya sheria, masuala ya ndoa na talaka, mirathi, wosia, sheria ya ardhi, haki za mtoto na namna ya kufanya utetezi yaani advocacy. Majimbo ambayo yamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika utekelezaji wa mpango huu ni pamoja na Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam, Jimbo Katoliki Same, Mbulu, Dodoma, Singida na Musoma. Hii imesaidia kupunguza kudharauliwa kwa mwanamke, na hivyo wanawake kupewa haki zao” ameeleza.
Pamoja na mafanikio hayo, amesema kuwa haki za mtoto mlemavu hazijastawishwa vizuri huku baadhi ya wazazi wakishindwa kuwapa watoto hao haki zao za msingi, na kusema kwamba Caritas inajipanga kundelea kuwaelimisha vizuri wazazi hao na kuwawezesha kiuchumi ili watoto wote wapate haki sawa.
Sambamba na kuwakomboa wanawake kiuchumi, Caritas imesaidia kupunguza unyanyasaji wa kijinsia ikiwa ni pamoja na vipigo kwa wanawake, ambapo limewajengea watanzania hali ya kuthamini na kujua umuhimu na thamani ya mtu mwingine huku mkazo ukiwekwa katika kuliishi Neno la Mungu.

“Tumewezesha usawa wa kijinsia

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI