SALA YA ASUBUHI. Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. SALA YA MATOLEO. Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina ...
Na Charles Rwehumbiza UINJILISHAJI BAGAMOYO NA TANZANIA KWA UJUMLA Kutokea Bagamoyo, wamisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu waliweza kuendelea kuinjilisha sehemu mbalimbali za Tanzania kama vile Mhonda (Morogoro), Mandera (Morogoro), Kilema Kibosho (Moshi) na Kondoa, n.k. Kutokana na ugumu wa watu wa Bagamoyo kukubali Injili na uamuzi wa wamisionari wenye asili ya Uholanzi kuhamia Morogoro mjini. Bagamoyo iliachwa kwa kipindi kirefu bila huduma za mapadri au wakiwa wanapata huduma ya Misa Takatifu mara moja kwa mwezi. Jambo hili lilisababisha ukuaji wa Kanisa la Bagamoyo kuwa duni sana hadi mwaka 1992 padri mwafrika wa kwanza alipoingia na kuweka makazi ya kudumu Bagamoyo. Padri huyu wa kwanza mwafrika kuinjilisha Bagamoyo sio mwingine ila Padrei Valentine Bayo wa Shirika la Roho Mtakatifu. Tangu aingie Bagamoyo, Padri Bayo chini ya usimamizi wa shirika lake, ameweza kuipa Bagamoyo hadhi iliyo nayo leo hii. Hakika haitakuwa vibaya kumwita Padri Bayo ...
J E, unazungumzaje kuhusu “chumaulete” ambapo inasemekana pesa za mtu mmoja zinaweza kwenda kwa mwingine kwa kufanya ushirikina? Jibu: Habari za “chumaulete” ni uongo wa kifukara. Ni uongo ambao kudhihirika kwake lazima ufikiri wa kinyume. Waafrika, katika dhiki zetu na ufukara wetu huwa na hadithi za kupata mali au pesa “kwa che”. Ndiyo kisa, kati yetu hustawi habari za kupata mali kwa uchawi au ushirikina, au kwa kutumia mapepo (yaani mashetani), au kwa kutumia majini, au kwa kupitia Frimasoni na kadhalika. Kila mara tuna maelezo ya ajabu kwa wanaokuwa matajiri kati yetu, yaani usiwe na nyumba au gari kuwazidi walio wengi mhali ulipo. Wengine tutasema ni wachawi. Wengine tutasema wanatumia mapepo au “majini” kama Waislamu waaminivyo. Wengine tutasema wanapata kwa kuwa ni wanachama wa Frimasoni na kadhalika. Kifupi, hatukosi maelezo sisi! Kumbe, kwa sababu ya dhiki zetu, Waafrika huwa tunaaminishana kwamba kuna njia za mikato za kupatia pesa au utajiri. Hiyo ndiyo imani in...
Comments
Post a Comment