SALA YA ASUBUHI. Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina. Ee Baba yetu Mungu mkuu, Umenilinda usiku huu. Nakushukuru kwa moyo, Ee Baba, Mwana na Roho. Nilinde tena siku hii, Niache dhambi, nikutii. Naomba sana Baba wee, Baraka zako nipokee. Bikira safi, Ee Maria Nisipotee nisimamie. Mlinzi mkuu malaika wee, Kwa Mungu wetu niombee Nitake nitende mema tu, Na mwisho nije kwako juu. Amina. NIA NJEMA. Kumheshimu Mungu wangu Namtolea roho yangu, Nifanye kazi nipumzike Amri zake tu nishike Wazo, neno, tendo lote Namtolea Mungu pote Roho, mwili chote changu, Pendo na uzima wangu Mungu wangu nitampenda, Wala dhambi sitatenda. Jina lako nasifia, Utakalo hutimia. Kwa utii navumilia Teso na matata pia. Nipe, Bwana, neema zako Niongeze sifa yako. Amina. SALA YA MATOLEO. Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie. BABA YETU. Baba yetu uliye mbinguni, jina
Na Charles Rwehumbiza UINJILISHAJI BAGAMOYO NA TANZANIA KWA UJUMLA Kutokea Bagamoyo, wamisionari wa Shirika la Roho Mtakatifu waliweza kuendelea kuinjilisha sehemu mbalimbali za Tanzania kama vile Mhonda (Morogoro), Mandera (Morogoro), Kilema Kibosho (Moshi) na Kondoa, n.k. Kutokana na ugumu wa watu wa Bagamoyo kukubali Injili na uamuzi wa wamisionari wenye asili ya Uholanzi kuhamia Morogoro mjini. Bagamoyo iliachwa kwa kipindi kirefu bila huduma za mapadri au wakiwa wanapata huduma ya Misa Takatifu mara moja kwa mwezi. Jambo hili lilisababisha ukuaji wa Kanisa la Bagamoyo kuwa duni sana hadi mwaka 1992 padri mwafrika wa kwanza alipoingia na kuweka makazi ya kudumu Bagamoyo. Padri huyu wa kwanza mwafrika kuinjilisha Bagamoyo sio mwingine ila Padrei Valentine Bayo wa Shirika la Roho Mtakatifu. Tangu aingie Bagamoyo, Padri Bayo chini ya usimamizi wa shirika lake, ameweza kuipa Bagamoyo hadhi iliyo nayo leo hii. Hakika haitakuwa vibaya kumwita Padri Bayo “ Baba wa Uinjilish
Na Philip Komba Utangulizi: Ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu ni moja ya ibada zinazojulikana sana katika Kanisa Katoliki. Ibada hii inauona Moyo wa Kibinadamu wa Yesu kama mwakilishi wa Mapendo yake ya Kimungu kwa wanadamu , na Kanisa nayo inaiona kama Mapendo na Huruma ya Yesu kwa wanadamu wote. Ibada ya Moyo Mtakatifu wa Yesu imefikia hatua hii tunayoishuhudia leo kutokana na maelekezo ya Mtakatifu Margareta Maria Alakok aliyejifunza uendelezaji wake wakati alipokuwa anatokewa na Yesu kwa mfululizo kati ya mwaka 1673 na mwaka 1675. Mtawa mwingine tena, Mwenyeheri Maria wa Moyo Mtakatifu (1863-1899), kutoka Chama cha Kitawa cha Mchungaji Mwema huko Ujerumani, aliisisimkia sana ibada hii baada ya kuwa na mazungumzo ya ana kwa ana na Yesu na akawahi hata kumwomba Papa Leo XIII, autolee ulimwengu wote kwa Moyo Mtakatifu wa Yesu kama alivyotumwa na Yesu. Wakati wa kipindi cha enzi ya kati, watangulizi wa ibada hii mpya, walijitokeza kutoka sehem
Comments
Post a Comment