"SAIDIENI WASEMINARI"
Waamini wa Jimbo Katoliki Kahama
wametakiwa kudumisha moyo wa kujitoa juu ya kuwasaidia
vijana wanaosoma shule ya seminari ya Ushirombo iliyopo parokia ya
Bikira Maria Msaada wa Daima kwa sababu ni kitalu na kitivo cha miito ya
upadri ndani ya Kanisa.
Wito huo umetolewa hivi karibuni na
Askofu wa Jimbo Katoliki Kahama, Mhashamu Ludovick Minde wakati wa harambee ya
kuichangia seminari ya Ushirombo na kutoa wito kwa waamini kuona hapo ndiyo
kitalu cha kupata miito ya upadri na maaskofu wa kesho.
Comments
Post a Comment