JIMBO KUU TABORA KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO CHA KIROHO KWA WAKATI

Jimbo Kuu Katoliki Tabora lipo katika mchakato wa kukamilisha ujenzi wa kituo cha Kiroho Kategile Tabora kwa ajili ya mapadri, watawa na walei jimboni humo.
Akiongea na blog hii katika mkutano uliofanyika katika eneo la Kituo hicho cha kiroho, Askofu Mkuu Paulo Ruzoka amesema Jimbo limeamua kujenga kituo hiki ili kujibu hitaji la kiroho kwa waamini wote wa Tabora ili kupata mahali pa kuinjilishwa zaidi.
Katika kukamilisha ujenzi huo, kila Parokia na Taasisi Jimboni Tabora zinaendelea kuchangia fedha, vifaa vya ujenzi na samani za ndani ili kukifanya kituo hicho kianze kutumika mwishoni mwa mwaka huu 2017.
Mpaka sasa kituo kimegharimu zaidi ya shilingi milioni 275 za kitanzania.  Askofu Mkuu amesema mpaka sasa majengo yaliyokwisha kamilika ni mabweni 2, kumbi 2 na nyumba watakayoishi mapadri na wahudumu wa kituo hicho.
Jimbo Kuu Tabora limeamua kujenga kituo hicho eneo hilo ili kuenzi historia ya miaka mingi ambapo zamani palitumika kama kituo cha mapumziko kwa waseminaristi wakubwa  baada ya kumaliza masomo yao katika Seminari Kuu ya Mt. Paulo Mtume Kipalapala  (1930-1955). 
Na baada ya mabadiliko kufanyika, waseminaristi waliruhusiwa kupumzikia maparokiani na pengine kupata nafasi ya kwenda kusalimia nyumbani kwa muda mfupi na kurudi parokiani (1956).
Kituo hicho kilifungwa baada ya baadhi ya miundombinu yake kutolewa na kupelekwa kwenye Parokia ya Ndono ambapo vilitumika katika ujenzi wa shule ya kati enzi hizo yaani middle school.  Mipango ikienda vizuri kituo kitaanza kutumika rasmi mwezi wa kumi mwaka huu. 
Kituo hiki kipo umbali wa Kilometa 30 toka makao makuu ya Jimbo kuelekea parokia ya Ulyankulu.






Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU