MATUKIO MBALIMBALI UFUNGUZI WA MKUTANO MKUU WA MAASKOFU WA MWAKA WA BARAZA LA MAASKOFU KATOLIKI TANZANIA, LEO KURASINI DSM
Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania TEC umefunguliwa leo Kurasini jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Baraza hilo, Askofu Mkuu Beatus Kinyaiya(aliyesimama). Mambo mbalimbali yatajadiliwa katika Mkutano huo ambao umebebwa na Tafakari Kuu ya "CHANGAMOTO ZINAZOKABILI FAMILIA". Awali, Katibu wa Balozi wa Baba Mtakatifu nchini, Mosinyori Daniel Pacho(kulia) ameshukuru ushirikiano mzuri anaopewa na Baraza la Maaskofu, na kubainisha kuwa Baba Mtakatifu anautambua ushirikiano huo naye ataendelea kutoa ushirikiano zaidi.
Comments
Post a Comment