“Fungeni kabla ya kupokea Ekaristi Takatifu”
Paroko wa parokia ya Chuo Kikuu Dsm Mlimani, Padri
Deograthias Mbiku amewataka wakristo kuiheshimu Ekaristi Takatifu kwa
kuzingatia kanuni wakati wa kuipokea.
Akizungumza na wakristo waliofurika katika Dominika ya Ekaristi
Takatifu katika Parokia ya Bikira Maria Konsolata
Kigamboni Dar es salaam, Monsinyori amesema kila mkristo inampasa kufunga saa
moja kabla ya kupokea Ekaristi Takatifu, na baada ya kupokea anaweza kuendelea
kula kadri atakavyo.
“Waamini wawe katika neema ya utakaso rohoni yaani mpokeaji
asiwe na dhambi ( 1 Paulo 11-27-32), wawe na usafi wa mwili, wawe
na imani ya kwenda kumpokea Mungu na mtu asile kitu chochote kabla ya kupokea isipokuwa
maji pekee.” Amebainisha.
Wakati huohuo Monsinyori ametoa sakramenti ya kipaimara kwa vijana
238 toka Parokia hiyo na kuwaagiza mambo ya kufanya ikiwa ni pamoja kumshuhudia
Kristo katika maisha yao, kutangaza habari njema kwa kila kiumbe na kwa kila Taifa,
wasome Biblia na kuijua wakiongozwa na Roho Mtakatifu waliyempokea, wasali kwa
bidii zote na watumie karama mbalimbali walizopewa na Mungu kwa maana kila
mwanadamu Mungu amempa karama zake.
Comments
Post a Comment