Serikali Mara kushirikiana na Kanisa Katoliki kuikabili njaa
SERIKALI Mkoani
Mara imesema alisema
kuwa suluhisho la tembo kuharibu mazao yakiwa ghalani limepatika kwani Serikali
itashirikiana na chuo cha
ufundi cha Mt. Antony
kuwahamasisha wananchi waweze kununua vihenge hivyo ambavyo tembo hawezi
kuharibu mazao yakiwa ghalani .
Hiyo ni moja ya mbinu ya kunusuru hali ya njaa inayowakabili
wananchi wa Mkoa huo kutokana na tembo kula mazao yakiwa shambani na hata baada
ya kuvunwa yakiwa ghalani.
Akizungumza kwenye mahafali ya 18 ya Chuo cha Ufundi cha Mt.
Antony kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma , yaliyofanyika
Chuoni hapo,Mkuu wa Mkoa wa Mara Dk Charles Mlingwa ambaye ndiye aliyekuwa
mgeni rasmi alisema kuwa amefurahishwa sana kuona vihenge
vya chuma vinavyotengenzwa Chuoni hapo vyenye uwezo wa kubeba
tani 2 kwa wakati mmoja.
“Mimi siamini kabisa kama tembo anaakili kumzidi binadamu na
ninashangaa sana kila mtu analalamikia tembo tembo imekuwa kama wimbo,lakini
baada ya kutembelea maeneo ya chuo hiki na kujionea shughuli za ufundi
mbalimbali zinazofanywa na chuo hiki nimefurahi sana na moja kwa moja nikaona
suluhisho la kilio cha wananchi kuhusu tembo nimekipata na sasa kilichobakia ni
uhamasishaji tu watu watumie vihenge hivi vya kisasa kuhufadhi chakula kuanzia
ngazi ya kaya,” alisema Dk Mlingwa.
Aidha ameahidi kushirkiana na chuo hicho katika kutatua changamoto
zinazokikabili chuo hicho na kusema kuwa chuo hicho ni kikubwa sana katika mkoa
huo na kinauwezo wa kuchukua wanafunzi wengi kwa kozi mbalimbali,wakati
wanaendelea na mchakato wa kujenga vyuo vingine.
Amelihakikishia
Kanisa kuwa, serikali itashirikana na
Chuo cha Ufundi cha Mt. Antony katika kufundisha mbinu za
kilimo cha nafaka, na kuboresha uhifadhi wa chakula kuanzia ngazi ya kaya ,kwa
kutumia vihenge vya kisasa vinayopatikana katika Chuo hicho ili kukabiliana na
tembo ambao wamekuwa wakiharibu chakula kikiwa ghalani.
Mkuu wa Chuo hicho Sista Rozina Kimaro alisema
kuwa jumla ya wahitimi 43 wamehitimu katika kozi mbalimbali,na hadi
sasa chuo hicho kimeshatoa wanafunzi 2392 wamehitimu mafunzi ya hao
wahitimu wapatao 610 wameajiliwa na wahitimu 940 wamejiajili wenyewe tangu
kianzishwe mwaka 1997 na hivyo kupunguza idadi ya vijana wasio na
ajira katika jamii.
Sista Kimaro alisema kuwa changamoto kubwa ambayo chuo inakabilana
nacho kwa sasa ni wafadhili kutoendelea kutoa msaada ,hivyo vijana ambao ni
yatima na wale wa mazingira magumu M,Kwaliokuwa wakisaidiwa
kutoendelea kusaidiwa tena kutokana na uwezo wa chuo kutoweza na ndoto zao
kudidimia.
Comments
Post a Comment