Ask. Minde awataka waamini kijiandaa kumpokea Mtoto Yesu.
ASKOFU Ludovick Minde wa Jimbo la Katoliki
Kahama amewataka waamini kujitakasa na kujiandaa kiroho katika kipindi
hiki cha maajilio ili waweze kumpokea kwa moyo
safi Masiha Yesu Kristo.
Askofu
Minde ametoa wito huo hivi karibuni katika Misa Takatifu alipokuwa
akizinduzia Parokia Teule ya Utatu Mtakatifu Lulembela
jimboni humo .
“Katika safari yetu ya
imani Mungu yupo kati yetu, kwa hiyo waumini tunapaswa kufungua mioyo
yetu ili aweze kutukirimia mambo makuu katika
matendo ya wokovu na ukombozi wetu
hasa wakati huu tunapoelekea kumpokea Masiha
Mkombozi wetu,” ameeleza.
Askofu Minde alisema
Parokia Teule ya Utatu Mtakatifu , Lulembela aliyoizindua ni moja
ya matunda ya Yubilee ya Mwaka wa Huruma ya
Mungu jimboni humo kwa kuwasogezea karibu waamini huduma
ya kiroho na kichungaji .
Alisema kuwa Parokia ya
Utatu Mtakatifu , Lulembela ina kilomita za mlaba
112 , senta 3 vigango 15 na jumla
ya waumini 2069 na imemegwa toka Parokia ya Bikira Maria Msaada
wa Daima Ushirombo na kuwataka waamini hao kubadilika
na kuachana na maisha ya zamani na kutimiza wajibu
wao kama parokia.
Ikumbukwe kuwa, hadi
sasa jimbo la Kahama lina jumla ya
parokia 23.
Comments
Post a Comment