Kard. Pengo ahimiza Watoto wafundishwe kuwa wamisionari wazalendo
ASKOFU Mkuu wa Jimbo Kuu
Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amehimiza wazazi,
jumuiya na Kanisa kwa ujumla kuwafundisha watoto kuwa wamisionari wazalendo ili
baadaye jamii ipate kizazi kinachoweza kuwajali wengine.
Kardinali
Pengo amesema hayo hivi karibuni alipoungana na Watoto wa Shirika la Kimisionari la Utoto Mtakatifu
Jimbo Kuu Dar es Salaam wa Dekania ya Ubungo na Kibaha walipowatembelea watoto yatima na wazee
wanaolelewa katika nyumba zao zilizopo Msimbazi
senta Dar es Salaam.
“Wamisionari
si wenye pesa tu, wamisionari hawatoki Ulaya. Mawazo hayo nadhani yameshatoka
katika mioyo ya waamini wetu hususani wa Dar es Salaam. Mmisionari ni mimi wewe
si lazima atoke ulaya. Kutoa msaada kwa wazee na watoto yatima ni kuonesha umisionari kati yetu.
Tunafahamu
kuwa watoto hawana kipato chochote lakini wanaweza kuwasaidia wengine kupitia
wazazi wao. Tunawalea katikamazingira ya kuona utu wa mwanadamu, thamani ya
wanadamu wengine hususani wenye shida. Wakiwa watu wazima watakuwa wanakumbuka
na tayari tumeshawaandaa kuwa na huruma kwa wenye shida. Hii ndiyo dhana ya
kuwapeleka kufanya matendo ya huruma kwa wenye shida mbalimbali. Tunalea kizazi
kinachojali wengine,” ameeleza Kardinali Pengo huku akisisitiza;
Leo
ni siku ya kufanya matendo ya huruma kwa wenye shida hususani katika kipindi
hiki cha majilio. Wale wenye dhiki na shida sisi Utoto Mtakatifu tunajitahidi
kufanya matendo ya huruma kwa wazee wasiojiweza, watoto wasio na wazazi.
Wote sisi wana utoto mtakatifu tunajihusisha
nao kwa lengo kubwa kwamba tunakua kwa pamoja kwa mawazo ya huruma na upendo.
Watot
wakizoea kufanya hivi wakiwawakubwa watasaidia wengne wenye mahitaji.
Maneno
waacheni watoto wadogo waje kwangu, ni maneno ya Kristo. Alipenda sana watoto
wadogo. Anatukumbusha upendo wa Kristo kwa watoto, watoto wajisikie wamefika
kwa Kristo mwenyewe.
Mara
kwa mara watoto wa utoto mtakatifu wanafanya matend ya huruma. Lengo letu kubwa
ni kuandaa wamisionari wa leo na siku za mbele katika taifa letu kwa moyo
uleule waliokuwa nao.
Tunapokuja
mahali kama hapa hususani kwenye kipindi cha maajilio, kuwahudumia hawa watoto
ni kwamba tungekuwepo Bethlehem tusingemuacha mtoto Yesu akazaliwa pangoni.
Tungempa nafasi nzuri. Sisi tunamhudumia Kristo kupitia watoto hawa wadogo
waliozaliwa wazazi wakafariki ama wakawatelekeza.”
Akizungumzia
juu ya watoto waliotelekezwa na wazazi wao, Kardinali Pengo amesema kuwa,Kwa
destiri watoto walotelekezwa ni ishara inayotia uchungu. Mtua anazaa mtoto
halafu anamtelekeza. Hata kama hana uwezo ina maana hana ndugu au jamaa. Watoto
pengine baba hajulikani mama anaona ugumu wa kumlea peke yake.
“Kweli
mtoto wa kike anaweza kuzaa mtoto tukashindwa kumlea? Hata kama si wa kabila
letu, rangi yetu na hatujui baba ni nani lakini tunao wajibu wa kuwalea watoto
hawa ili wasitelekezwe ama kuuawa.
Ni
wazi kuna wanaopata watoto katika mazingira yasiyoeleweka. Tuna wajibu wa
kuwalea na kuwasaidia. Ndiyo maana ninasisitiza kuwa lazima kila mtu walau awe
na jumuiya yake, akiwa ana matatizo jumuiya haipaswi kumtupa nje, imsahihishe
asiharibike.
Wengine
wanawaua, kuwatupa kwenye maji machafu, mazingira mabaya nk. Haya yanatokea kwa
mabinti wetu. Lazima tuwakemee kwa yale
wanayofanya lakini tuwajengee mazingira ya kujiepusha na hatari hizo.
Ndiyo
maana Kanisa linawalea watoto wa Utoto Mtakatifu ili wakue katika maadili ya
Kikristo,” ameeleza.
Amewahimiza
wale wanaowalea watoto hao yatima kuwa wanapaswa kusimamia na kuwalea watoto
katika maadili na wajitoe kwa moyo wote.
“Waacheni
watoto wadogo…. Hawa wanasimama badala ya kristo mwenyewe.
Kristo
hakuwafukuza, aliwakumbatia na kuwabariki. Kupitia wao, watoto wajisiskie
wanapendwa na Kristo.
Aidha
amewahimiza waamini kujitoa kuwalea watoto na wazee kwani ni jukumu lao.
Wasiiache serikali na Kanisa.
Kwa
upande wake mzee Peter Matimbwa (78) amemshukuru Kardinali Pengo pamoja na
watoto wa Utoto Mtakatifu kwa zawadi walizowapatia nakusali pamoja nao.
Watoto
hao walitoa fedha taslimu milioni 2 na vitu mbalimbali vyenye thamani y ash.
Milioni 1.338.
Comments
Post a Comment