Askofu Nzigilwa: furaha na amani havipatikani katika Mali

PAMOJA na mali nyingi alizokuwa nazo Adamu Mungu aliona bado kuna  jambo la msingi ambalo Adamu alikuwa akilihitaji katika maisha ambalo ni tofauti kabisa na mali pamoja na fahari zote alizokuwa nazo, hivyo akaona ni vema ampatie msaidizi,
Hayo yamesemwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es salaam Mhasham Eusebius Nzigilwa katika Homilia yake wakati wa Ashimisho la sadaka ya misa Takatifu  ambayo Brigedia Mstaafu Joachim Ngonyani  alikuwa akimshukuru Mungu  kwa kutimiza miaka 50 ya Ndoa iliyofanyika katikaKkanisa la Mtakatifu Peter Ostabay jijini Dar Es Salam.

Katika Ibada hiyo, Askofu Nzigilwa alisisitiza kuwa  Mungu alimleta mwanamke  kuwa makusudi ili aweze kumsaidia mume katika safari yake ya maisha ya hapa duniani. Hivyo ili ndoa idumu ni wanaume kuwapenda wake zao, ili kuwe na furaha ndani ya familia zao.
 
Akieelezea ndoa ya Brigedia Ngonyani na Mama Ewada alisema kuwa ni ndoa ya kuigwa na kila wanajamii wote huku akimpongeza Mkewe ambaye ameishi kwa miaka 35 na mume wake akiwa kwenye kiti baada ya kupata ajali ambayo ilimuacha na ulemavu wa miguu na bila kuchoka akaendelea kuishi na mumewe kwa kuzingatia kiapo cha ndoa yao



Kwa Upande wake Brigedia Ngonyani amemshukuru Mungu kwa miaka 50 ya ndoa yao,  pia amemshukuru baba Askofu Nzigilwa kwa Ibada ya Misa Takatifu,  huku akitoa siri ya kufikia hapo alipo kuwa ni Upenda, Msamaha na Uvumilivu.

Familia ya Brigedia Ngonyani imebahatika kuwa na Watoto watano wa kike, wawili na wakiume watatu na wajukuu zaidi ya 20.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

MJUE MTAKATIFU MARIA GORETTI