SAUT yafanya Mahafali ya 18
CHUO
Kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza (SAUT) ambacho kinamilikiwa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania kinafanya
mahafali yake ya 18 tangu kuanzishwa kwake.
Akizungumza katika mkutano na waandishi
wa habari uliohudhuriwa na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari nchini,
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Padri Dkt, Thaddeus Mkamwa amesema sherehe hizo za
mahafali zinafanyika kwa siku mbili yaani Desemba 16 na 17 mwaka huu.
Amebainisha kuwa takribani
wahitimu 3000 wa vitivo mbalimbali wanahitimu
kwa nyanja tofauti na kuwa wamegawanya mahafali hayo kwa siku mbili kwa ajili
ya wingi wa wanafunzi na kurahisisha shughuli hiyo.
Mgeni rasmi ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza Mhashamu Thaddeus Ruwaichi ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Vyuo Vikuu Katoliki Tanzania ambaye
anamwakilisha Mkuu wa Chuo hicho yaani (Chancellor) Askofu Tarcisius
Ngalalekumtwa ambaye ni Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania na pia
Askofu wa Jimbo la Iringa.
Katika mkutano huo Padri Dokta
Mkamwa ameongeza kua mahafali hayo yametanguliwa na siku ya maonesho ya chuo
ambayo yanajulikana kama (SAUT community day) yaliyofanyika Novemba 14 katika
uwanja wa chuo hicho ali maarufu kwa jina la Raila Odinga ambapo wanafunzi
pamoja na wahadhiri wao watashiriki katika maonesho hayo mbalimbali kutoka
katika kila kitivo na idara huku wakijumuika na jamii inayowazunguka.
“ SAUT inajivunia mafanikio
yake kuanzia kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1998 ikijulikana kama Nyegezi (Social
Training) kabla hakijabadilishwa kuitwa SAUT,ambapo kilianza na wahitimu 102 na
mpaka sasa takribani kimeweza kuhitimisha takribani wanafunzi 30,000 tangu
kuanzishwa kwake.
Chuo kimejitahidi kuweka elimu
sawa kwa wanafunzi wote wa kike na wakiume na pia kua kimekua na mahusiano
mazuri na mataifa mbalimbali kutoka nchi za nje,na kua kwa mwaka huu wa masomo
2016/2017 SAUT kimeweza kupokea wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali yakiwemo China, Ujerumani, Finland,
Marekanina Canada ambapo wanafunzi hao wanakuja kujifunza chini ya makubariano
kati ya SAUT na vyuo vyao (Bilateral agreements),” ameeleza Padri Mkamwa.
Aidha ameeleza kuwa, chuo hicho
pia kinafundisha masomo ya lugha za nje ikiwemo kifaransa na kichina kwa walimu,
wanafunzi na wafanyakazi. Hivyo amewasihi watu wengi wajitokeze kusoma kichina ili
waweze kukabiliana na soko la ajira kwa kuzingatia China sasa ni taifa lenye
guvu kiuchumi duniani.
Ameongeza kua katika mafanikio
hayo pia chuo kinajivunia kutoa wanafunzi imara na shupavu na pia wenye nidhamu
watakao enda kulitumikia taifa kwa Nyanja zote, na kua wanafunzi wote kutoka
katika program mbalimbali wameshiriki mafunzo yako katika mafunzo ya vitendo
kwa taasisi na mashirika mbalimbali.
Vilevile amesema kuwa mwaka huu
chuo hicho kina wahitimu watatu wa shahada ya uzamili (PhD) wakitokea katika
kitivo cha sayansi ya mahusiano ya umma yaani PhD in mass communication.
Aidha amebainisha kua takribani
wanafunzi 746 hawataweza kuhitimu katika mahafari hayo kwa sababu zao binafsi
ikiwemo kukosa sifa za kuhitimu yaani
kutofanya vizuri katika masomo yao, wengine kuahirisha mwaka na pia kushindwa
kufanya mtihani yao kwa sababu ya kiuchumi.
Aidha amebainisha changamoto
mbalimbali zinazokikumba chuo hicho ukiwemo uhitaji wa vifaa vya kufundishia
mfano vifaa tiba na uhandisi, ukosefu wa wachangiaji yaani wanafunzi na
serikali pale wanapochelewa kutoa ada kwa wakati na pia asilimia chache ya
wanafunzi ambao wanakua hawapo tayari kusoma na kusababisha idadi ya wanafunzi wanaoshindwa
kuhitimu kuongezeka.
Hivyo kutokana na changamoto
hizo inalazimu chuo kutafuta pesa za ziada kuendelea kufundisha na kutoa
wanafunzi walio bora.
Katika mahafali hayo ya 18
tangu kuanzishwa kwake yamebebwa na ujumbe ‘Changia katika mchango wa SAUT
katika kuandaa nakutoa wahitimu bora na mahili kwa jamii.’
SAUT ni chuo kikuu cha katoliki
ambacho tangu kuanzishwa kwake kimeweza kuzaa takribani vyuo vitatu ambavyo
mpaka sasa vinajitegemea yaani MWECAU,
RUCU na CUHAS Bugando
Comments
Post a Comment