Barua ya Papa Francisko kwa Rais Bashar Al Assad wa Siria
Baba Mtakatifu Francisko kwa kumteuwa na hatimaye kumsimika
Askofu mkuu Mario Zenari kuwa Kardinali, alitaka kuonesha kwa namna ya pekee,
upendo wake kwa wananchi wa Siria ambao kwa takribani miaka mitano wamekuwa
wakiteseka kutokana na vita.
Baba Mtakatifu kwa njia ya Kardinali Mario Zenari,
Balozi wa Vatican nchini Siria amemtumia barua Rais Bashar al Assad, akimwomba
pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kusaidia mchakato wa kusitisha vita nchini Siria
kwa kujikita katika mchakato wa majadiliano yatakayosaidia kurejesha tena
maridhiano kati ya watu kwa kuondokana na chuki na fitina kati yao.
Baba Mtakatifu analaani misimamo mikali ya kidini na kiimani kwa
kumwomba Rais Bashar Al Assad kuhakikisha kwamba, sheria za kimataifa
zinaheshimiwa mintarafu ulinzi na usalama kwa raia pamoja na kuhakikisha
kwamba, waathirika wanafikiwa na misaada ya kimataifa!
Comments
Post a Comment