“Mpelekeni Yesu katika mazingira ya shule”
“KUMPELEKA Yesu katika mazingira ya shuleni
iwe ni sehemu ya maisha yenu ya kila siku ili kupitia ninyi wanafunzi wezenu
wamuone Yesu.
Jinsi
mnavyovaa, mnavyoshirikiana, mnavyofwata sheria za shule, mnavyofanya ibada na
mnavyosoma kwa bidii. Kuwavute vijana wengine na kuwa na matamanio ya kuishi
kama ninyi. Huko ndiko kumhubiri Kristo katika mazingira yenu.”
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania Padri Raymond
Saba wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa (TYCS) uliofanyika Kurasini, Jijini Dar
es salaam.
Padri
Saba amesisitiza vijana kuwa wanatakiwa kujituma kutafuta ufumbuzi wa matatizo inayowazunguka
ili muweza kuyatatua.
Msali
rozari kila siku sio mnazivaa tu hizo rozari na kutembea nazo kwani kuvaa bila
kusali ni sawa na hirizi. Msimtafute Mama Bikira Maria kipindi cha matatizo tu
bali msali rozari kila siku hivyo ndivyo Mama Bikira Maria alivyotutaka tufanye.
TYCS
mnatakiwa kujiendesha wenyewe kwani bado mnayonafasi angalieni namna gani
mnaweza kujiendesha bila kutegemea wafadhili .
Ningependa
siku moja kuwaona mkiwa viongozi wakubwa katika nchi hii, wakubwa kwa namna ya
kuwatumikia watu vizuri kwa haki na usawa kwa kufuata sharia,” amesema Padri
Saba.
Pia
aliwashukuru walezi kwani wametoa muda wao kuwasindikiza vijana katika mkutano
wao wa kufanya uchaguzi mkuu wa kuwapata viongozi pia kuwalea kwenye maadili
mema huku akiwasisitiza walezi wengine wawalee vijana vizuri katika malezi ya
kila siku.
Mratibu
wa vijana Taifa Padri Liberatus Kadio ametoa shukrani kwa viongozi na walezi
waliofika kwenye mkutano huo wa uchaguzi wa mwaka. Pia amewapongeza viongozi
waliomaliza muda wao wa uongozi akisisitiza kuwa, bado wanahitajika kiutendaji
mpaka kongamano la vijana litakapomalizika mwakani.
Comments
Post a Comment