SHIVYAWATA laitaka Serikali kufanya sensa ya walemavu
Rai hiyo imetolewa hivi karibuni na watu wenye ulemavu katika maazimisho ya siku ya walemavu ambayo huazimishwa Desemba 3 kila mwaka duniani ambapo kwa mkoa wa Singida yamefanyika wilayani Manyoni
Lengo la maadhimisho hayo ni
kuhamasisha jamii, serikali na wadau mbalimbali kutambua uwezo uliopo kwa watu
wenye ulemavu na kujenga mazingira ya kushiriki katika shughuli mbalimbali
za maendeleo.
Walemavu hao wamesema iwapo serikali itafanya sensa itaweza kujua idadi ya walemavu waliopo ikiwa ni pamoja na kujua mahitaji muhimu yanayotengwa na serikali ili kuwatosheleza walengwa wa makundi yote.

Shirikisho la vyama vya watu
wenye ulemavu limemuomba kupitia risala yao mkuu wa mkoa wa Singida kutatua
changamoto zinazolikabili shirikisho hilo. Awali akisoma risala fupi kwa mgeni
rasmi aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Singida, Mwenyekiti wa halmashauri ya
wilaya ya Manyoni shirikisho
Changamoto hizo ni pamoja na kutokupata nafasi za ajira kwa watu wenye ulemavu, kutokuwepo kwa kamati za watu wenye ulemavu, kutokuwepo kwa ofisi ya shirikisho mkoa, kofia pamoja na miwani ya kuzuia jua bado ni changamoto kwa walemavu wa ngozi, miundo mbinu kwa walemavu wa viungo pamoja na alama za kufundishia kwa walemavu wa macho.

Bwana Moses Matonya
aliyemuwakilisha mkuu wa mkoa wa Singida amesema serikali ya mkoa itaendelea
kushirikiana nao na kutatua changamoto walizozieleza ili kuhakikisha maendeleo
ya watu wenye ulemavu kwa mkoa huo yanastawi kwa hali ya juu.
Aidha Matonya ametoa rai kwa walemavu hao kutowabagua wenzao kikabila ama kidini bali washirikiane na kujenga umoja katika shughuli mbalimbali za maendeleo.
Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) ni muunganiko wa vyama vitano yaani chama cha walemavu wa macho, chama cha walemavu wa ngozi, chama cha viziwi, chama cha walemavu wa akili na chama cha wenye ulemavu wa viungo .
Na Dotto Kwilasa, Manyoni-Singida.

Comments
Post a Comment