Waamini watakiwa kuwa makini na maendeleo ya teknolojia
WAAMINI wametakiwa kuwa
makini juu ya maendeleo ya sayansi na teknolojia
yanayoendelea duniani kote
yasije yakawaondoa katika misingi wa imani
waliyonayo ndani ya Kanisa.
Hayo yamezungumzwa
na Askofu Ludovick Minde wa Jimbo Katoliki Kahama alipokuwa akifunga mwezi wa
Rozali Takatifu katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Karoli Lwanga parokia ya Kahama
mjini.
“ Wakristo sasa
hivi katika maisha yetu tumezingirwa na mambo mengi katika dunia hii ya sayansi
na teknolojia mnapaswa kuwa waagalifu na kusimama imara katika mafundisho na mapokeo ya Kanisa,” Amesema
Askofu Minde.
Askofu Minde
aliwataka waumini kukufua moyo wa sala kwa Mama Bikra Maria kwa kila muumini ,
familia , jumuiya na kwa Kanisa lote katika shida mbalimbali wataweza
kushuhudia makuu kwenye maisha yetu ya kila siku.
Alisema sala ya
Rozali Takatifu ni alama ya kumshukuru Mungu
kwa zawadi ya Mama Bikra Maria anayetujali fadhili nyingi binafsi katika mioyoni mwetu , amani familia,
jumuiya, taifa letu na
kwa kanisa kwa ujumla.
Askofu Minde katika
kufunga mwezi wa sala ya Rozali Takatifu
aliwaongoza waamini wa Kanisa Kuu
la parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga
Kahama mjini kusali rozali mafungu yote
kwa maandamo na kisha kumaliza kwa ibada huku akiwaalika kuwa watu wa sala kwa
Kristo na Mungu wetu katika kupata wokovu.
Comments
Post a Comment