Papa: Wanawake Mapadri Kanisa Katoliki hapana
Asisitiza Karismatiki
kufwata taratibu za Kanisa Katoliki
Vatikani
KIONGOZI wa Kanisa Katoliki
duniani Papa Fransisko amesema, Kanisa Katoliki halitaruhusu kuwa na wanawake
mapadri ijapokuwa linaheshimu nafasi ya wanawake katika maendeleo ya Kanisa.
Amesema
hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa kwenye msafara wake
nchini Swedeni, Novemba 1, 2016.
Katika
msafara huo Papa Fransisko alizungumzia kuhusu Wakimbizi na wahamiaji; Daraja
Takatifu ya Upadri kwa wanawake na msimamo wa Kanisa Katoliki; Majadiliano ya
kiekumene na Kanisa la Kiorthodox, Kanisa Anglikani na Kanisa la Kiinjili la
Kiluteri Duniani; Amani, upatanisho na umoja wa kitaifa nchini Venezuela.
Pia
amezungumzia Changamoto ya ukanimungu Barani Ulaya; biashara haramu ya binadamu
na utumwa mamboleo .
Baba
Mtakatifu amewashukuru na kuwapongeza waandishi wa habari waliokuwa kwenye
msafara wake kwa kazi nyeti waliyoifanya wakati wa Sala na ushuhuda wa
kiekumene kati ya Waluteri na Wakatoliki.
Baba
Mtakatifu ametumia fursa hiyo, kuwashukuru wananchi wa Swedeni ambao wamekuwa
na utamaduni wa upendo na ukarimu kwa wakimbizi na wahamiaji, kiasi kwamba,
takwimu zinaonesha kwamba. Nchini humo kuna wakimbizi na wahamiaji wapatao
millioni 9 na wengi wao wanatarajiwa kupewa uraia wa Sweden.
Wanawake mapadri hapana
Baba
Mtakatifu anasema, msimamo wa Kanisa Katoliki kuhusu Daraja Takatifu ya Upadri
kwa wanawake, ulikwisha kutolewa na Mtakatifu Yohane Paulo II na hakuna
mabadiliko yoyote juu ya hilo.
Kuhusu
uwezo wa wanawake katika kutekeleza dhamana na wajibu wao kama Mapadri na
Maaskofu, anasema, hana uhakika na mchuano mkali kati ya wanawake mapadre na
wanaume mapadri!
Wanawake
wana karama na mapaji ambayo wakiyatumia vyema na kwa uaminifu wanaweza kufanya
vyema zaidi hata kuliko wanaume.
Haya
ni mambo ambayo yanaweza kuchambuliwa katika nyaraka mbali mbali za maisha na
utume wa Kanisa.
Mtakatifu
Petro ni mkuu wa kikosi kizima cha Mitume waliokabidhiwa dhamana ya kutangaza
na kushuhudia Habari Njema ya Wokovu hadi miisho ya dunia.
Mwelekeo
wa Bikira Maria ni ushuhuda wa dhamana na utume wa wanawake katika ustawi na
maendeleo ya Kanisa la Kristo. Wakati wa Pentekoste, Bikira Maria alikuwa
pamoja na Mitume wa Yesu.
Kanisa
ni Mama na mwalimu na hakuna Kanisa bila ya kuwa na mwelekeo huu wa Kimama!
Wanawake wana nafasi kubwa katika kuliendeleza Kanisa kutokana na karama na
nafasi zao lakini si lazima wawe mapadri kwani hata Kristo hakuchagua mitume 12
wanawake.
Ekumene
Baba Mtakatifu anasema,
Mwaka 2016 umefunikwa na matukio mengi ya majadiliano ya kiekumene kati ya
Kanisa Katoliki, Kanisa la Kiorthodox, Kanisa la Kianglikani pamoja na Kanisa
la Kiinjili la Kiluteri Duniani. Ni matumaini yake kwamba, ataendelea kushiriki
kikamilifu katika mchakato wa majadiliano ya kiekumene yanayosimikwa katika
uhalisia wa maisha ya waamini kama alivyofanya alipowatembelea waamini wa
Kanisa la Kipentekosti mjini Caserta, nchini Italia. Kanisa Katoliki kwa miaka
mingi halikuwatendea haki waamini wa Makanisa ya Kipentekosti, kumbe, hapa kuna
haja ya kuomba msamaha na kuanza mchakato wa kuganga na kuponya madonda ya
utengano, chuki na uhasama kati ya waamini. Baba Mtakatifu anasema, anapenda
kuendeleza mchakato wa majadiliano ya kiekumene kwani ni sehemu ya vinasaba vya
maisha na utume wake. Majadiliano katika maisha ni chachu muhimu sana inayoweza
kudumisha majadiliano katika ngazi mbali mbali ili kujenga utamaduni wa
kufahamiana, kuheshimiana na kuthaminiana kama ndugu wamoja katika Kristo Yesu.
Azungumzia kuhusu Karesmatiki
Chama cha Kikatoliki cha
Uhamsho wa Roho Mtakatifu kwa kushirikiana na Chama cha Wakarisimatiki
Wakatoliki kunako Mwaka 2017 wanaadhimisha Jubilei ya miaka 50 ya uwepo na
utume wao ndani ya Kanisa; matunda ya maadhimisho ya Mtaguso Mkuu wa Pili wa
Vatikani. Vyama hivi wakati wa Mkesha wa Pentekosti vitafanya kongamano la
kimataifa naye anatarajiwa kushiriki kikamilifu.
Baba Mtakatifu anawataka
waandishi wa habari kuwa makini na matumizi ya Neno “Pentekosti” kwani linaweza
kuleta utata kidogo!
Baba
Mtakatifu anasema, Chama cha Wakarisimatiki Wakatoliki kilipoanzishwa nchini
Argentina, alikuwa wa kwanza kukipinga kwamba, alitamani kuona Liturujia
ikiheshimiwa na wala si kugeuka kuwa ni shule na mahali ambapo waamini walikuwa
wanaendesha ibada zao kama makanisa ya kipentekosti!
Lakini
leo hii, anamang’amuzi na mwelekeo na mtazamo tofauti kabisa, kwani taratibu
aliweza kugundua tunu bora katika maisha na utume wa Wakarisimatiki Wakatoliki
kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya Kanisa la Kristo LAKINI KWA KUFWATA TARATIBU ZA KANISA KATOLIKI.
Kuhusu
wakimbizi na wahamiaji
Baba Mtakatifu anakaza
kusema, kuna haja ya kutofautisha kati ya wakimbizi na wahamiaji. Wakimbizi ni
watu wanaolazimika kuzikimbia nchi zao kwa sababu mbali mbali na wanayo haki ya
kimataifa inayowalinda na kuwasimamia ili waweze kupata hifadhi na usalama wa
maisha yao.
Ni watu wanaokimbia vita,
dhuluma na nyanyaso; baa la njaa na majanga asilia yanayotokana na athari za
mabadiliko ya tabianchi. Wakimbizi wanahitaji msaada, huduma na fursa za ajira.
Nchini Sweden, wakimbizi wamepewa kipaumbele cha pekee na Serikali katika
kuwasaidia kujifunza, utamaduni na mapokeo ya wananchi wa Sweden.
Baba Mtakatifu anakumbusha
kwamba, Bara la Ulaya limejengeka kutokana na watu kutoka katika makabila,
lugha na tamaduni mbali mbali.
Anasikitika kuona kwamba,
kuna baadhi ya nchi za Ulaya zinazojikita katika sera ya uchoyo kwa kutaka
kufunga mipaka ya nchi zao, badala ya kuwa wazi na wakarimu kwa kubainisha sera
na miakati ya kuwapokea na kuwapatia hifadhi bora ya maisha. Kila nchi
iwajibike kadiri ya uwezo na rasilimali iliyopo. Wakimbizi na wahamiaji
wasipopata hifadhi, wanatumbukizwa katika utumwa mamboleo na matokeo yake hata
utamaduni unadumaa kutokana na woga na hofu isiyokuwa na mashiko!
Hapa
Baba Mtakatifu anawataka wakuu wa nchi kujivika fadhila ya busara, ili
kuhakikisha kwamba, wakimbizi na wahamiaji wanapata fursa ya watoto wao kwenda
shule, kupata matibabu msingi, makazi bora na salama pamoja na fursa ya kazi.
Sweden ni mfano bora wa kuigwa katika kuwapokea, kuwahifadhi na kuwahudumia
wakimbizi na wahamiaji.
To be frank it is much better for the christian community + other communities vatcan II number 322-326 by Aloisius Daniel Babati Manyara
ReplyDelete