BIASHARA YA BINADAMU IKOMESHWE-PAPA

Ni matumaini ya Baba Mtakatifu Fransisko kwamba mkutano mkuu wa Pili wa Mtandao wa Mashirika ya Kitawa Barani Ulaya dhidi ya biashara haramu ya binadamu na unyonyaji, RENATE kuanzia tarehe 7 – 11 Novemba 2016 itakuwa ni fursa ya kusali, kutafakari na kufanya upembuzi yakinifu, utakaozaa matunda kwa wakati wake. Huu ni mkutano unaofanyika mjini Roma, wakati huu, Mama Kanisa anapoendelea kuadhimisha Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya huruma ya Mungu, kipindi cha neema na mwaliko wa kuzama katika huruma ya Mungu, kama Wasamaria wema, ili kuganga na kuponya madonda ya mwanadamu katika ulimwengu mamboleo kwa mafuta ya huruma ya Mungu.

Comments

Popular posts from this blog

SALA YA ASUBUHI:SALI HIVI..

Ujio wa Wamisionari wa Kwanza Tanzania Bara (2)

HISTORIA YA SHEREHE YA MOYO MTAKATIFU WA YESU